
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora ACP Suzan Kaganda
Na Hastin Liumba, BrotherDanny BlogNzega: KATIKA Hali isiyo ya kawaida Bibi kikongwe Mkwezi Masanja (75) mkazi wa Kitongoji cha Majengo majarubani kata ya Nzega Mjini wilayani Nzega Mkoani Tabora amejinyonga mpaka kufa kwa kutumia nguo aina ya khanga akiwa nyumbani kwake.
Akizungumza na waandishi wa Habari Mtoto wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Kawawa Manaa alisema tukio hilo lilitokea majira ya saa 4 usiku wa kumakia Disemba 5, mwaka huu.
Alisema mama yake alitoka nje kujisaidia na hakurudi ndani mpaka hapo majirani walipoona mwili wake ukinin`ginia chini ya mti.
Alisema sababu za kujinyonga kwa bibi huyo ni kutokana na ulemavu wa akili aliokuwa nao ambapo hapo awari aliwahi kuondoka nyumbani hapo na kupatikana katika vijiji jirani.
Alisema kuwa bibi huyo alikuwa hana ugomvi na mtu yeyote nyumbani hapo hata hivyo aliongeza kuwa hali yake ya kuchanganyikiwa ilikuwa ikijitokeza kwa nyakati tofauti tofauti hapo nyumbani.
Baadhi ya majirani wakizungumzia tukio hilo walisema kuwa waliona mwili ukining`nia chini ya mti na ndipo watu walijitokeza kutoa taarifa polisi.
Akizungumza kwa njia ya simu yake ya mkononi kamanda wapoli mkoani Tabora Suzan Kaganda alisema kuwa taarifa hizo zimefika ofisini na wanafanya uchunguzi wa tukio hilo.
*Imeandaliwa na www.brotherdanny5.blogspot.com
No comments:
Post a Comment