Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 11 December 2014

HII NDIYO BAISKELI YA DHAHABU INAYOUZWA SH. 600 MILIONI


Ni rahisi sana kwa watu kulalamikia gharama ya kununua baiskeli wengi wakitaka bei nafuu. Nyingi ya baiskeli nchini Uingereza huuzwa kwa Pauni 1,000 (sawa na Sh. 2.4 milioni za Tanzania).
Kwa wengi nchini humo hizo ni pesa nyingi sana.
Hata hivyo baikeli mpya iliyotengezwa kwa dhahabu imezinduliwa nchini humo. Bei yake? Pauni 250,000 au Sh. 600 milioni pesa za Tanzania. Bei hii ni ghali hata kuliko bei ya gari jipya la Ferari, kukufahamisha tu.
Gia za baiskeli hii zimetengezwa kwa dhahabu
Baiskeli hio ambayo ilitengezwa na kampuni ambayo hutengeza vitu vya kifahari, Goldgenie imetengezwa kwa dhahabu kutoka kwa mikono na vyuma vyake vyote. Kiwango cha dhahabu iliyotumiwa ni karati 24.
Wataalamu wa kampuni hio ya Goldgenie, wameweka dhahabu katika vyuma vya baiskeli hio vyote , mnyororo na mfumo unaofanya baiskeli kwenda na kubadilisha gia vyote vimewekwa dhahabu.
Mkurugenzi wa kampuni iliyotengeza baiskeli hii anasema inaweza kuendeshwa kwa barabara kama baiskeli nyinginezo
Na wakati baiskeli hio inavutia macho, inapowekwa nyuma ya kabati ya glasi na kulindwa na walinzi. Mkrugenzi wa kampuni hio anasema baiskeli hio inaweza kuendeshwa kwenye barabara.
"baiskeli hii sio tu ya kuvutia macho, bali pia ni nzuri ya kuendesha ikiwa mwenye kuiendesha atsatahimili kuangaliwa sana.''
Muundo wa baiskeli hii ni wa hali ya juu,'' aliongeza kusema mkurugenzi huyo.
Kwa sasa haijulikani idadi ya baiskeli hizo zitakazotengezwa, lakini ikiwa utakuwa na bahati sana unweza kupata moja kama hio. Lakini itakubidi ununue kufuli kuifungia baiskeli yako ikiwa hautakuwepo ambako umeiwacha.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment