Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 4 December 2014

HALMASHAURI 80 KUPEWA MILIONI 500 KWA AJILI YA NYUMBA ZA WALIMU

Dk. Shukuru Kawambwa

Na Mwandishi Wetu, BrotherDannyBlog
Arusha: HALMASHAURI 80 nchini zimetengewa kiasi cha shilingi milioni 500 kwa mwaka huu  kwa ajili ya  kujengea nyumba za walimu ili kuhakikisha walimu  wanaachana na nyumba za kupanga mitaani.



Aidha kwa mwaka jana halmashauri 40 ambazo zilikuwa kwenye hali mbaya za kutokuwa na nyumba za walimu tayari zimeshanufaika na mpango huo ambao utasaidia kwa kiwango kikubwa kuinua viwango vya ufaulu hapa nchini.

Hayo yalisemwa jana na waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi dr Shukuru Kawambwa alipokuwa akizungumza na wadau wa elimu katika uzinduzi rasmi wa shule ya sekondari Olmotony Forest iliyopo wilayani Arumeru.

Dr Shukuru alisema kuwa tatizo la nyumba za walimu limekuwa changamoto kubwa inayoikabili kila eneo na hili kuhakikisha kuwa tatizo hilo linaisha serikali imeamua kuanzisha mpango huo wa kuangalia halamashauri ambazo ziko katika hali mbaya ili kuwezesha walimu waishi katika mazingira magumu.

“Nyumba za walimu zimekuwa wimbo wa kila siku ili kuondokana na tatizo hili serikali yetu imeamua kuhakikisha kuwa hizi halmasahuri 80 kuanzia mwaka huu zinapata milioni 500 ili kujengea nyuma za walimu nah ii itasaidia zaidi hata walimu kukaa karibu na watoto,” aliongeza.

Aliongeza kuwa tatizo la walimu kupangisha mitaani na kukaa mbali na wanafunzi nayo ni moja ya changamoto ambayo inarudisha nyuma kiwango cha ufaulu kwani walimu hujikuta wakitembea umbali mkubwa hadi shuleni na kufika wakiwa wamechoka jamabo ambalo uwafanya kufundisha kwa kujilazimisha.

Hata hivyo alidai kuwa serikali imeweka mpango wa kuhakikiasha kuwa walimu wanatatuliwa matatizo yao yote ikiwemo kupatiwa motisha pamoja na kulipa madeni yote wanayodai ili kuziwezesha shule kufikia mpango wa matokeo makubwa sasa( BRN).

Awali mkuu wa shule hiyo Anna Minja  akisoma risala kwa mgeni rasmi alisema kuwa shule hiyo ilianzishwa mwaka  2013 ambapo ujenzi wa shule hiyo umegharimu jumla ya shilingi za kitanzania milioni 328.

No comments:

Post a Comment