Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 9 December 2014

CHADEMA YAWAONYA VIJANA KUTOGEUZE UONGOZI DILI



Na Hastin Liumba, BrotherDanny Blog

Nzega: UMOJA wa Katiba ya Wananchi (UKAWA)  wilayani Nzega mkoani Tabora umewataka vijana kutotumika kama daraja la kupata viongozi wabovu wasiokuwa na sifa kwa jamii kutokana na kutumia pesa chafu kuomba nafasiza uongozi.

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Nzega Omary  Omary katika  uzinduzi wa kampeni  za uchaguzi wa serikali  za mitaa zinazoendelea  sehemu mbalimbali hapa hapa wilayani.
Alisema kuwa vijana wanapaswa kuwa makini katika kipindi hiki cha uchaguzi kutokana na kuwepo na wimbi la viongozi wabovu.
Alisema baadhi ya viongozi na vyama hutegemea vijana kuwapatia pesa chafu ilikupata kura zao huku wakishindwa kuchagua viongozi wenye uwezo wa kuongoza.
Alisema vijana wasigeuze kipindi hiki chaguzi kuwa ni Dili  badala yake wawe makini kuchagua viongozi wenye kuweza kuwatetea kwa muda wa miaka mitano iajayo ukilinganisha na changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo.
‘’Vijana msIgeuze uchaguzi ni Dili hapana uchaguzi ni jambo kubwa sana ndio msingi wa maisha ya Taifa nawaombeni sana kuepuka viongozi wanaotoa pesa kwani hao ni viongozi wabovu chagueni viongozi wa UKAWA ambao hawana pesa hao ndio watawaletea maendeleo," alisema Omary Omary.
Diwani wa kata ya Nzega Mjini (CUF) Dominck  Clement Kizwalo akiwanadi wagombea wa Umoja huo alisema kuwa  viongozi wabovu hutumia kuwapikia vyakula vijana hususani wali na nyama wakitegemea kupigiwa kura.
Alisema vijana ndio wanakumbana na changamoto za maisha ikiwa kufukuzwa katika maeneo ya kufanyia kazi ikiwa na kukosa fursa mbalimbali za kufanya maendeleo sababu ya kula wali na nyama za viongozi wanao wachagua.
Kizwalo alisema ni wakati umefika wakufanya mabadiliko ya kuchagua viongozi makini ambao wanatokana na umoja huo UKAWA ilikupata maendeleo bora kwa jamii.katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa ambpo .
‘’Msinunuliwe kwa wali nyama na soda hapana tumieni busara na hekima katika kuchagua viongozi umoja wetu umeweka viongozi sehem zote na nimakini hivyo chagueni umoja wa ukawa ,hatuna wali nyama na soda ila ahadi zetu ni kuleta maendeleo’’alisema kizwalo.

*Imeandaliwa na www.brotherdanny5.blogspot.com

No comments:

Post a Comment