Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh.
Anastazia Wambura akimsikiliza kiongozi wa msafara wa Asasi za Kiraia toka mkoani Mtwara Dkt.
Lillac Malumbo aliyesimama wakati asasi hizo zilipomtembelea ofisini kwake kwa
lengo la kubadilishana mawazo juu ya mila na desturi zilizopitwa na wakati za
mkoa huo. (Picha na Benjamin Sawe-WHUSM).
Katibu wa msafara Bi. Rhobi Elias akisoma risala kwa
mgeni rasmi hayupo pichani kuhusiana na mila na desturi hatarishi na
zilizopitwa na wakati zinazoendelea kutumika katika Mkoa wa Mtwara, mila hizo
ni pamoja na kuwapeleka watoto wa kike kwenye unyago wakiwa na umri mdogo, na
ndoa za umri mdogo.
(Picha na Benjamin
Sawe-WHUSM).
Katibu wa msafara Bi. Rhobi Elias kushoto
akimkabidhi risala Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh.
Anastazia Wambura inayoelezea mila na desturi hatarishi na zilizopitwa na
wakati zinazoendelea kutumika katika Mkoa wa Mtwara, mila hizo ni pamoja na
kuwapeleka watoto wa kike kwenye unyago wakiwa na umri mdogo, na ndoa za umri
mdogo. (Picha na Benjamin Sawe-WHUSM)
No comments:
Post a Comment