Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 16 February 2016

DRFA YAIPONGEZA AFRICAN LYON KUREJEA LIGI KUU KWA KISHINDO MSIMU UJAO, 2016/17.


Chama cha soka mkoa wa Dar es Salaam DRFA, kimeeleza kufurahishwa kwake na hatua iliyofikiwa na klabu ya African Lyon ya kurejea katika Ligi Kuu soka Tanzania Bara msimu wa mwaka 2016/2017,baada ya kumaliza wa kwanza katika kundi lao la “A” wakiwa na pointi 27.Lyon imefikia hatua hiyo baada ya kushinda mechi 8 na kutoka sare mechi 3 kati ya mechi 14 ilizocheza, na kuiacha nyuma pointi 2 klabu ya KMC FC iliyomaliza katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 25.
Mwenyekiti wa DRFA, Almas Kasongo,amelipongeza benchi zima la ufundi la Lyon pamoja na uongozi kwa ujumla,kwa juhudi za kuendelea kuung’arisha mkoa wa Dar es salaam kisoka.
Kasongo pia amezipongeza timu za Ashanti United iliyomaliza katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 24, Friends Rangers iliyomaliza katika nafasi ya nne ikiwa na pointi 23,pamoja na Polisi Dar es salaam iliyomaliza katika nafasi ya 6 ikiwa na pointi 14 zote za Dar es salaam,kwa uthubutu wao wa kujaribu kutinga ligi kuu.
Michuano ya ligi daraja la kwanza kwa msimu huu wa mwaka 2015/2016,ilishirikisha jumla ya timu 24 zilizopangwa katika makundi matatu yenye timu nane kila kundi,huku kila kundi likitakiwa kutoa timu moja kuingia ligi kuu.

Timu nyingine iliyopanda ligi kuu ni pamoja na maafande wa Ruvu Shooting ya mlandizi mkoani pwani iliyomaliza wa kwanza katika kundi “B” wakijikusanyia pointi 33,huku katika kundi la “C” uamuzi wa Tff unasubiriwa baada ya klabu za Polisi Tabora na Geita Gold fc,zote kumaliza wakiwa wamefungana pointi 30.

No comments:

Post a Comment