Mkuu
wa Kituo cha Uhamiaji mpakani Tarakea, wilayani Rombo Mkoa wa Kilimanjaro, John
Kapembe akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja
Jenerali Projest Rwegasira (wapili kushoto aliyevaa kiraia) eneo la Tanzania
katika mpaka huo uliopakana na nchi ya Kenya. Rwegasira yupo mkoani humo kwa
ziara ya kikazi akitembelea vituo vya Uhamiaji vya mipakani mkoani humo. Picha
zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Afisa
Uhamiaji Mkoa (RIO) wa Kilimanjaro, Naibu Kamishna Ambrose Mwanguku (kulia)
akimkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali
Projest Rwegasira (wapili kulia) wakati alipowasili katika Jengo la Kituo cha
Pamoja cha huduma mpakani Holili, wilayani Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro kwa ajili
ya ziara ya kikazi ya kutembelea mipaka ya Uhamiaji mkoani humo Watatu kulia ni
Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli.
Kaimu
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli akimkaribisha Katibu Mkuu wa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati
meza kuu) azungumze na Maafisa wa Idara ya mbalimbali za Serikali wanaotoa
huduma katika Kituo cha Pamoja cha Huduma Mipakani Holili wilayani Rombo, Mkoa
wa Kilimanjaro. Rwegasira aliwataka maafisa hao wafanye kazi kwa ushirikiano ili
kuiletea maendeleo nchi yao.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira
(katikati meza kuu) akizungumza na Maafisa wa Idara ya mbalimbali za Serikali
wanaotoa huduma katika Kituo cha Pamoja cha Huduma Mipakani cha Holili,
wilayani Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro. Meja Jenerali Rwegasira katika hotuba yake
aliwataka maafisa hao wafanye kazi kwa ushirikiano ili kuiletea maendeleo nchi
yao.
Kaimu
Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji mpakani Holili, Edwin Mwasota akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (watatu kulia) moja ya ofisi zilizopo
katika Jengo la Kituo cha Pamoja cha Huduma Mipakani cha Holili, wilayani
Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro. Wapili kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa
Uhamiaji, Victoria Lembeli. Meja Jenerali Rwegasira alifanya ziara ya kikazi
kwa kutembelea vituo vya Uhamiaji vya mipakani mkoani Kilimanjaro.
Afisa
Uhamiaji Mkoa (RIO) wa Kilimanjaro, Naibu Kamishna Ambrose Mwanguku (kushoto)
akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali
Projest Rwegasira (wapili kushoto) mpaka Tanzania pamoja na Jengo la Uhamiaji
la nchini Kenya (Taveta) wakati walipokuwa juu ya ghorofa ya Jengo la Kituo cha
Pamoja cha Huduma Mipakani Holili, wilayani Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira
(wapili kushoto aliyevaa kiraia) akiondoka katika Jengo la Kituo cha Pamoja cha
Huduma Mipakani Holili, wilayani Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro mara baada ya
kumaliza ziara yake ya kulitembelea jengo hilo na kuzungumza na maafisa
mbalimbali wa serikali wanaotoa huduma za mpakani mkoani humo. Kushoto ni Afisa
Uhamiaji Mkoa (RIO) wa Kilimanjaro, Naibu Kamishna Ambrose Mwanguku na Kulia ni
Afisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika mpakani Holili, Aden
Mwakalobo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment