Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 14 February 2016

ACACIA STAND UNITED YAINGIA KAMBINI KUWAVIZIA MAAFANDE WA JKT RUVU


Timu ya Acacia Stand United 'Chama la Wana' inayodhaminiwa na kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Acacia Gold, mara baada ya kupoteza mchezo wake wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa kufungwa goli 2-1 na  Simba, kesho Jumatatu inataraji kuingia kambini katika Mgodi wa Dhahabu Buzwagi kujiandaa na mchezo wake unaofuata dhidi ya Maafande wa jeshi la kujenga taifa JKT Ruvu.
Ofisa Habari wa klabu hiyo Isaac Edward amesema kupoteza mchezo wao dhidi ya Simba ni sehemu ya matokeo ya soka, kwani hivi sasa ligi ni ngumu na kila timu inapambana ili kupata matokeo mazuri.
“Tumepoteza mchezo wetu tukiwa nyumbani dhidi ya Simba ni sehemu ya mchezo, tunajipanga na mchezo unaofuata nyumbani ambao tutacheza na JKT Ruvu, timu inatarajia kuingia kambini kesho Jumatatu katika Hosteli za Mgodi wa Dhahabu Buzwagi kujiandaa na mchezo wetu unaofuata.”
Ameongeza kuwa mchezo ujao timu hiyo ya Acacia Stand United imejipanga kuhakikisha inapata ushindi ili wazidi kujiweka sehemu nzuri kwenye msimamo wa ligi kuu  Tanzania Bara.
“Uongozi pamoja na Benchi la Ufundi tumejipanga vilivyo ili tupate pointi tatu ambazo zitazidi kutuweka katika nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi,” alisema.
Isaac amewaomba mashabiki na wapenzi wa klabu hiyo kuunganisha nguvu kwa pamoja na kuisaidia timu kupata matokeo mazuri nyumbani na ugenini.
“Mashabiki wetu na wapenzi wa Acacia Stand United 'Chama la Wana' waendelee kuipa timu ushirikiano katika michezo yetu yote iliyobaki katika mzunguko wa pili ambao ni wa lala salama ikiwa tunacheza nyumbani na hata ugenini pia”.
Acacia Stand United FC kwasasa imejikusanyia pointi 29 katika michezo yake 18 walioshuka dimbani katika msimu huu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

No comments:

Post a Comment