Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 12 May 2015

WINROCK INTERNATIONAL WAPONGEZWA

 

Na Hastin Liumba, Sikonge
SERIKALI wilayani Sikonge mkoani Tabora imepongeza Shirika la Winrock International kupitia mradi wake wa PROSPER unaotekelezwa mkoani Tabora kwa jitihada zake kubwa za kuwezesha akinamama kiuchumi na kutokomeza vitendo vya utumikishwaji watoto mashambani.


Mkuu wa wilaya ya Sikonge Hanifa Selengu alitoa pongezi hizo kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo toka nchini Marekani Rodney Fugerson  alipotembelea wilaya hiyo kukagua miradi mbalimbali ya kijamii iliyofadhiliwa na Shirika hilo kupitia mradi wa PROSPER.

Selengu alisema wilaya yake inajivunia  miradi ya kijamii iliyofadhiliwa na shirika hilo kwani imekuwa mkombozi kwa wananchi wake hususani akinamama, vijana na watoto waliokuwa wakitumikishwa mashamba ya tumbaku.

 Alieleza mradi huo umewainua akinamama kiuchumi kwani wengi wao walikuwa wakiishi maisha duni wakitegemea kilimo cha tumbaku pekee hali iliyowafanya washindwe kupeleka watoto shule.

 ‘Kama serikali tunajitahidi kuboresha maisha ya wananchi wetu ikiwemo kiuchumi lakini pekee yetu hatuwezi kufanikiwa kwa asilimia 100, kwani bado tunakabiliwa na changamoto katika mstakabali mzima wa kuwaletea maendeleo wananchi ,’, alisema.

 Aidha Selengu alimwomba Mtendaji huyo Mkuu wa shirika kuongeza mkataba wa mradi huo hapa nchini kwani bado wanauhitaji kutokana na kukabiliwa na changamoto zaidi zinazohitaji msaada wa shirika hilo, mradi huo ulianza kutekelezwa wilayani humo mwezi Juni 2011 na unatarajiwa kumalizika mwezi Desemba mwaka huu.

Naye Vick Walker ambaye ni Meneja Mkuu wa Miradi ya Shirika hilo aliyeambatana na Rodney toka nchini Marekani alipongeza uongozi wa wilaya hiyo kwa jinsi ulivyosimamia vizuri utekelezaji wa miradi ya PROSPER.
  

No comments:

Post a Comment