Tarehe 30 Mei 2015, Dar es Salaam, Wadhamini wa shindano la Fanya Kweli Kiwanjani “Tusker Lager” mali ya Kampuni ya bia ya Serengeti wamemuibua mshindi wa tatu wa shindano hilo siku ya jumamosi baada ya mtanange mkali wa kuitafuta baa ya wiki uliofanywa na wadhamini hao wiki iliyopita.
“New Jambo Bar” ya Mabibo, Ubungo ndiyo iliyobahatika kuzipiga kikumbo baa nyingine 9 zilizoingia kwenye mchakato huo wa kumpata mshindi wa wiki.
Kama ilivyo ada siku ya jumamosi mameneja wa bia ya Tusker waliweka kambi katika kiwanja cha New Jambo Bar ya Mabibo jijini Dar na kuporomosha burudani ya nguvu sambamba na kugawa zawadi mbalimbali kama fulana, fedha taslim na bia za bure kwa wapenzi wa bia ya Tusker hii ikiwa ni sehemu ya kurudisha fadhila kwa wateja wa kinywaji hicho waliofika kupongeza ushindi wa baa hiyo.
Burudani ya kuipongeza “New Jambo Bar” kama baa ya wiki ilianza mishale ya saa kumi na moja na kudumu kwa takriban masaa sita. Burudani hiyo ya muziki ambayo ilikua ikirushwa laivu na kituo cha redio cha E-fm ni muendelezo wa sherehe mbalimbali zinazofanywa na Tusker kwenye baa mbalimbali za jiji la Dar ambazo zimeshinda shindano la “Fanya Kweli Kiwanjani”.
Akiisifia baa yake, alipokuwa akihojiwa na waandishi wa habari, Bw. Frank David Lema ambaye ndiye Meneja wa baa hiyo alisema “Nimefurahi sana kwa watu wa Tusker kututembelea kwenye baa yetu kwa kweli leo tumeuza kupita kiasi”. Kwa kweli natamani hata wiki ijayo wangeendelea kuichagua tena baa yetu aliongeza Meneja huyo huku akicheka na kumalizia kuwa wameuza chapa hiyo ya Tusker kuliko siku zote tangu baa hiyo ifunguliwe kutokana na wingi wa wapenzi wa kinywaji hicho.
Kwa upande wake Afisa Mauzo wa SBL, eneo la manzese – Mabibo, Bi. Anna Msomba ambaye alikuwepo kiwanjani hapo alisema kuwa “Tumefurahi kumpata mshindi wa tatu wa shindano letu, “New Jambo baa” ni baa nzuri na ya kistaaarabu yenye wapenzi wengi wa Tusker na nadhani hii ndiyo sababu kubwa ya watu kuipigia kura baa hii…Kampeni hii bado inaendelea na tunatarajia zaidi ya baa 20 kuingia kwenye kinyang’anyiro hiki kabla ya promosheni kufikia tamati”.
Bi. Msomba aliendelea kuwasihi wadau na wapenzi wa bia ya Tusker kuendelea kuzipigia kura baa mbalimbali zitakazo orodheshwa kwenye shindano hilo na kukumbushia kuwa ili kuziwezesha baa za mitaa tunayoishi kuingia kwenye shindano hili wasisite kusikiliza kipindi cha Ubaoni cha E-fm ambacho kinadadavua kwa undani kuhusiana na promosheni hiyo.
Pamoja na hayo, Meneja huyo alikabidhi Tsh. 100,000Tsh fedha taslim kwa wahudumu wa baa hiyo kama zawadi kwa kufanya kweli kwenye upande wa kutoa huduma kwa siku hiyo.
No comments:
Post a Comment