FIFA, shirikisho lenye utajiri wa mabilioni ya dola za Kimarekani ambalo linasimamia mchezo wa soka duniani,limekumbwa na kashfa ya rushwa kwa miongo mingi, ambapo maafisa wa ngazi ya juu wa soka walikamatwa mapema Jumatano.
Huku viongozi wa FIFA wakikutana mjini Zurich, Jumatano, maafisa wa polisi waliwasili katika hoteli moja ya nyota tano ya Baur au Lac kuwakamata baadhi ya maafisa wa ngazi ya juu wa shirikisho hilo la soka duniani kwa ombi la wizara ya sheria ya Marekani.
Bwana Blazer alikiri kosa mwaka 2013 kwa makosa 10, iikiwa ni pamoja na ulaghai, udanganyifu wa fedha kupitia mtandao na njama za kutenda makosa na kulipa faini ya dola milioni 1.9za Kimarekani.
Watu wengine watatu - wakiwemo watoto wawili wa kiume wa afisa wa soka kutoka eneo la Caribbean Jack Warner - pia kampuni mbili za masoko za masuala ya michezo pia zilikiri makosa.
• Katika mkutano wa waandishi wa habari mjini Zurich, msemaji wa FIFA amesema hali ilikuwa nzuri kwa shirikisho lake kwa sababu ilionyesha kuwa FIFA ina shauku ya kubadilika. Pia amesema shirikisho hilo haitafungua mchakato wa maombi ya kuandaa fainali za mwaka 2018 na 2022, japokuwa maafisa wa Uswisi wamesema wafungua uchunguzi sambamba na kukamata nyaraka na data za kielektroniki kuhusiana na masuala hayo.
• Mwanasheria Mkuu wa Marekani Loretta E. Lynch, ambaye aliingia madarakani mwezi uli na Mkurugenzi wa F.B.I. James Comey wanatarajiwa kuitisha mkutano wa waandishi wa habari Jumatano saa 04:30 asubuhi mjini Brooklyn.
Nani wanashitakiwa?
Jeffrey Webb: Rais wa shirikisho la soka kwa vyama vya Amerika ya Kati Concacaf, moja ya mashirikisho sita ya kimaeneo yanayounda shirikisho la FIFA, na makamu rais wa FIFA.
Jack Warner: Rais wa zamani wa Concacaf na makamu wa rais wa FIFA.
Eugenio Figueredo: Rais wa zamani wa Conmebol, shirikisho la soka la Amerika Kusini na makamu wa rais anayemaliza muda wake.
Eduardo Li: Rais wa shirikisho la Costa Rica, alikuwa tayari kujiunga katika kamati ya utendaji ya FIFA wiki hii.
Julio Rocha: Rais wa chama cha soka cha Nicaragua
Costas Takkas: Rais wa zamani wa shirikisho la kandanda la Visiwa vya Cayman.
Rafael Esquivel: Rais wa chama cha soka cha Venezuela tangu mwaka 1988
José Maria Marin: Rais wa zamani wa shirikisho la Brazil
Nicolás Leoz: Rais wa zamani wa Conmebol na mjumbe wa zamani wa kamati ya utendaji ya FIFA.
Alejandro Burzaco: Afisa mtendaji wa michezo katika vyombo vya habari nchini Argentina
Aaron Davidson: Rais wa Traffic Sports nchini Marekani - mdhamini wa matukio ya michezo- na mwenyekiti wa bodi ya Ligi ya Soka Amerika Kaskazini
Hugo Jinkis: Afisa mtendaji wa michezo katika vyombo vya habari.
Mariano Jinkis: Afisa mtendaji wa michezo katika vyombo vya habari
José Margulies: Ameshitakiwa kwa kufanikisha malipo kinyume cha sheria.
Nini kuhusu Sepp Blatter?
Sepp Blatter, rais wa FIFA tangu mwaka 1998, hajafunguliwa mashitaka, japokuwa maafisa wa soka ambao wameshitakiwa huenda wakawasilisha taarifa muhimu kwa waendesha mashitaka, ambazo zinaweza kumharibia Bwana Blatter katika azma yake ya kutaka kuchaguliwa tena kwa mara ya tano kuwa rais wa FIFA. Uchaguzi uliopangwa kufanyika Ijumaa mjini Zurich, unaonekana kumpa Bwana Blatter awamu ya tano kama rais.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment