Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday, 31 May 2015

WACHIMBAJI WADOGO WACHANGAMKIA MIKOPO NSSF

Na Hastin Liumba, Nzega
BAADHI ya wachimbaji wadogo wa dhahabu wilayani Nzega mkoani Tabora wamejiandaa kujiunga  na Shirika la Taifa la Hifadhi ya jamii(NSSF) baada ya kupatiwa mafunzo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika mgodi mdogo wa Isunga walisema  Taasisi hiyo inapaswa kutoa Elimu kubwa kwa kundi hilo ambalo halipati taarifa muhimu kama hizo ambazo zinaweza kuwanufaisha.

Yohana Rameck alisema  wachimbaji wengi wameitikia wito wakujiunga na Nssf na kuiomba taasisi hiyo izidi kutoa Elimu ya kutosha kwa jamii iliwaweze kujuinga.
Alisema  wachimbaji wadogo wamekuwa wakifanya kazi kwa mazingira magumu kazini bila kujua wapi watapata sehemu ya kukidhi mahitaji yao na kuongeza kuwa  Elimu hiyo iweze kusambazwa kwa haraka iliwaweze kupata mikopo.

Kwaupande wake Mwenyekiti wa  chama cha wachimbaji wadogo mkoani Tabora Taborema,Rashidi  Shabout alisema  wachimbaji wengi watajiunga na mfuko huo ambao utaweza kunufaisha katika Nyanja mbalimbali za kimaisha.

Shabout alisema endapo wachimbaji wakajiunga vikundi na kuingia katika mchakato huo wataweza kupatiwa mikopo kwa riba nafuu ambayo itarahisisha kazi zao na kupata vifaa mbalimbali vya kisasa vitakavyo  weza  kuwaongezea  vipato.

Meneja wa Nssf  wilaya ya Nzega na Igunga Martin  Madadi alisema kuwa  Taasisi hiyo inaendelea na uhamasishaji kwa wajasilia mali wote ilikuhakikisha wanapata fursa hiyo muhimu  ambayo itaongeza hali ya maisha yao.

Alisema kuwa wakijiunga na mfuko huo watapa matibabu bure ikiwa na mafao ya uzeeni na fursa mbalimbali zilizopo katika mfuko huo.

Aliwataka waajili wote wa sekta binafsi kuhakikisha wanafuata sheria  katika kuhakikisha kila mfanya kazi anajiunga na mfuko wa hifadhi ya jamii ilikuweza kujikwamua kimaisha ikiwa na kupata furusa.

No comments:

Post a Comment