Vikosi mbali mbali ya Majeshi vikiwa vimejipanga tayari kwa kungia uwanjani kwa ajili ya ufunguzi wa michezo ya majeshi 2015.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni mkuu wa Wilaya ya Songea Prof. Nomarn Sigalla King akisalimiana na wachezaji wa timu ya jeshi kutoka Mtwara.
.........................................
Na Amon
Mtega ,SONGEA
MICHEZO ya
majeshi inayoshirikisha vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama briged ya kanda
ya kusini imefunguliwa rasmi na kaimu mkuu wa mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni mkuu
wa wilaya ya Songea ,Pr Noman sigaa King huku benki ya NMB tawi la Songea
likiwa limetoa msaada wa jezi za mpira wa miguu seti saba ambazo zenye thamani
ya shilingi 3,000,000.
Akiongea
kwenye ufunguzi huo uliyofanyika leo katika uwanja wa michezo wa
majimaji uliyopo Songea ,Sigara alisema kuwa
michezo hiyo itaimarisha mahusiano ya kiulinzi baina ya mipaka yetu ya
Tanzania kwa kuwa vyombo vyote vya ulinzi na usalama vitakuwa na ushirikiano.
Alisema kuwa
ulinzi wa Tanzania katika mipaka yetu
hautegemei jeshi moja tuu bali ni ushirikiano wa vikosi vya majeshi
mbalimbali kama vikosi hivi ambavyo vimeshirikishwa kwenye michezo hii
iliyozinduliwa na ambayo itarajiwa kufanyika kwa wiki mbili.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Prof. Norman Sigalla King akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya The Might Elephant .
....................................................
Aidha Pr,
Noman alizitaka taasisi za kifedha zilizopo hapa nchini kuwamstari wa mbele
katika kudumisha mahusiano ya mambo mbalimbali ikiwemo ya michezo kwa kuwatoa
misaada kama ilivyo kwa benki ya NMB.
“Taasisi za
kifedha zinauwezo mkubwa wa kutoa misaada ya ushirikiano kwa kuwa zimekuwa na
frunsa nyingi katika kufanikisha
mahitaji yanayotakiwa na wahitaji “alisema Noman Sigara ambaye ni kaimu
mkuu wa mkoa wa Ruvuma.
Kwa upande wake kamanda Briged ya Tembo kanda
ya kusini John Chacha awali kabla ya uzinduzi huo alisema kuwa licha ya
kufanyika kwa michezo ya mpira wa miguu pamoja na mpira wa pete na wa kikapu toka
kwenye vikosi mbalimbali vinavyoshiriki alisema kuwa kutakuwemo na mchezo wa
kulenga shabaha ambao alidai kuwa ni mhimu kwa upande wa jeshi hilo.
Chacha
alisema kuwa mchezo wa ulengaji shabaa ni mchezo mhimu sana kwa jeshi kwa kuwa
ndio unaomfanya mwanajeshi kuwa tayari mda wote katika utendaji wao wa kazi
ambao huendana na shughuli hizo.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Prof. Norman Sigalla King akionyesha ufundi wake wa kumiliki mpira katika ufunguzi wa michezo ya majeshi.
.......................
Kwa upande wake meneja wa benki ya NMB tawi la
Songea Rehema Nasib akikabidhi msaada
huo wa jezi alisema kuwa benki hiyo imejijengea utaratibu wa kuungana na jamii
katika kutekeleza mambo mbalimbali ambayo yanayo hitajika.
Rehema alisema kuwa licha ya benki hiyo
kujijengea tabia hiyo lakini bado imekuwa ikithamini michango inoayotolewa na
jamii pamoja na jeshi kwa kuwa wamekuwa wateja wakubwa ndani ya benki hiyo.
Katika
michezo hiyo zaida ya vikosi tisa vinashiriki michezo hiyo na tayari imeshaanza
kuchezwa katika uwanja wa maji maji.
Baadhi ya washiriki wakifatilia mchezo
Katoka kulia kwako wa pili ni Katibu wa SUFA akifatilia mashindano ya majeshi na wa kwanza kulia kwako ni mtangazaji wa Jogoo FM Bw. Onesmo Emilani.
No comments:
Post a Comment