Haya ni machimbo ya dhahabu ya Nsungwa mkoani Tabora.
Na Hastin Liumba, Nzega
KAMPUNI ya uchimbaji dhahabu ya Ilalo Gold Mining iliyopo Kijiji cha Ilalo, Kata ya Igusule wilayani Nzega mkoani Tabora imesema itashirikiana na wananchi kuimarisha ulinzi na usalama.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa kuimaimarisha uhusiano mwema na wanakijiji Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Sultan Mohamed Sultan alisema kampuni hiyo itakuwa bega kwa bega na serikali ya kijiji.
Alisema katika kijiji hicho pamekuwepo matukio ya utekaji wa magari ya abiria ikiwa ni pamoja na wananchi wanaotumia barabara hiyo hali inayosababisha kupunguza shuguli za uzalishaji mali.
Katika kuimarisha ulinzi na usalama Mkurugenzi, huyo alikabidhi simu tano za mkononi ambazo zitaweza kudumisha mawasiliano ya ulinzi na kukabiliana na wahalifu.

Akipokea msaada huo wa simu tano za mkononi Mbunge wa Jimbo la Bukene Sellemani Zedi alisema wananchi wanapaswa kuimarisha ulinzi kwa kushirikiana na kampuni hiyo ili kukomesha hali hiyo.
Alisema kampuni hiyo imekuwa na mahusiano mazuri na wananchi ikiwa ni pamoja na kujali wajibu wake ilikuweza kupunguza migogoro ambayo ingeweza kupatikana.
Zedi alisema kuwa wananchi wanapaswa kuimarisha ulinzi kwa kutumia jeshi la jadi la sungusungu ambalo litapiga doria kila sehemu ili kuweka hali ya usalama kijijini hapo.
Aliongekuwa kijiji hicho kinapaswa kushirikiana na jeshi la polis wilaya kwa mawasiliano ikiwa na kutoa taarifa pindi wanapo wahisi watu ambao wanaweza kuwa wahalifu.

No comments:
Post a Comment