Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Juma Assad
NA SALOME KITOMARY
Taasisi tano za serikali zimeisababishia serikali hasara ya Sh. bilioni 10 kwa kipindi cha miaka miwili.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Juma Assad (pichani), ya mwaka 2013/14 inaonyesha uwapo wa mashaka makubwa juu ya uwezo wa taasisi hizo kuendelea kujiendesha endapo hatua za makusudi hazitachukuliwa na serikali katika kuzinusuru.
Taasisi hizo ni Taaisi ya teknolojia Dar es Salaam (DIT), Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB), Chama cha hakimiliki na Hakishirikishi Tanzania (Cosota), Chuo Kikuu Huria (OUT) na TFC.
Kiasi cha hasara kwenye mabano kwa kila taasisi kwa mwaka 2011/12, DIT ( Bil 1.5), TFC (Bil 1.58), TDB (Mil 58.145), mwaka 2012/13 ni DIT (Mil 68.4), TFC (bil 3.7), OUT (bil 1.09), TDB (Mil 75.903) na Cosota (Mil 231.1).
Aidha, CAG amebaini mapungufu katika mradi wa ujenzi wa jengo la ‘Linear Accelerator Treatment’ katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road wa Sh. Bil 3.333.
Taarifa hiyo imebainisha kuwa kwa mujibu wa mkataba huu, ujenzi ulitakiwa kumalizika ndani ya wiki 32, lakini hadi kufikia Disemba 16, 2014, kazi pekee iliyokamilika ni maandalizi ya eneo la ujenzi.
“Kiasi cha fedha kilichokuwa kimelipwa kwa mujibu wa hati ya malipo kilikuwa Sh. milioni 349 ikijumuisha bima na malipo ya awali,” ilifafanua.
CAG alibainisha kuwa kwa mujibu wa Menejimenti ya Taasisi ya ORCI mkataba huo ulitekelezwa kwa kuzingatia bajeti iliyotengwa ya Sh. bilioni nane kutoka serikalini na hakuna kiasi chochote
kilicho kuwa kimepokelewa kwa kipindi cha mwaka wa fedha.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment