
Hii ni Shule ya Sekondari ya Wavulana Tabora
Na Hastin Liumba, Tabora
MRATIBU wa Mtandao wa Elimu Tanzania TEN/MET Cathleen Sekwao amewataka wazazi mkoani Tabora kubadilika na kulipa suala la elimu kipaumbele ili kunusuru anguko la elimu mkoani humo.
Akizungumza katika kilele cha Maadhimisho ya wiki ya elimu Mkoani hapa Sekwao alionyesha dhahiri kusikitishwa na hali ya kiwango cha elimu mkoani hapa jambo ambalo amesema linachangiwa na mwamko duni wa wazazi.
Alisema licha ya wazazi wengi kukabiliwa na hali ngumu ya maisha na umaskini uliokithiri katika familia nyingi Mkoani hapa hali iliyochangia kwa kiasi kikubwa utoro sugu wa wanafunzi mashuleni kutokana na watoto wengi kulazimika kutafuta vibarua ili kuweza kuijikimu kimaisha.
‘Wazazi wengi bado wana mwamko duni, wanapaswa kuwahimiza watoto wao kuhudhuria shuleni hali ili kuchochea maendeleo ya zaidi kielimu, aliongeza.
Alisema katika maadhimisho haya wameweza kubaini changamto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo mkoani hapa ikiwemo umbali wa shule ambapo watoto hutembea zaidi ya kilometa 12 kwa siku na kuchelewa vipindi kila siku.
Aidha aliongeza changamoto nyingine inayozikabili shule za msingi na sekondari ni vijiwe vya 'pulltable', kamali na vibarua katika mashamba ya tumbaku ikiwa ni pamoja na wasichana kujipeleka kwa wanaume hali inayosababisha mimba.
Sekwao aliongeza uongozi wa Serikali wa ngazi ya chini pia umekuwa kikwazo hasa kutokana na kesi za utoro na mimba za utotoni na kushindwa kutoa maamuzi juu.
Mkuu wa wilaya ya Tabora Suleiman Kumchaya aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa amewaagiza Wakurugenzi wote wa Halmashauri za Mkoa wa Tabora kuhakikisha wanawachukuliwa hataua kali pamoja na kuwafiksha katika vyombo vya sheria wale wote watakao bainikia kuwa kikwazo cha elimu kwa watoto wao.
No comments:
Post a Comment