Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 12 May 2015

TAMBUA SOKWE NA WANYAMA WAISHIO HIFADHI YA GOMBE

Displaying Gremlin na mwanae Gizzimo. Mama aliezaa mapacha (Golden na Glitter)..JPG
Sparrow (57) sokwe mwenye umri mkubwa Gombe. Ni mama wa Sandi na bibi wa Siri.
Displaying DSC01640.JPG

Sehemu ya milima ya hifadhi ya Taifa Gombe mkoani Kigoma
Displaying DSC01691.JPG
Nyani walioko Hifadhi ya Taifa Gombe
Displaying DSC01738.JPG
Maporomo ya Kakombe yaliyoko ndani ya Hifadhi ya Taifa Gombe mkoani Kigoma (Picha zote na Hastin Liumba).
Displaying Mama ( Sandi) mtoto (Siri)..JPG
Mama ( Sandi) na mtoto (Siri) hawa wote wapo katika hifadhi ya Taifa Gombe.
Displaying Sparrow (57) sokwe mwenye umri mkubwa Gombe. Ni mama wa Sandi na bibi wa Siri..JPG
Gremlin na mwanae Gizzimo. Mama aliezaa mapacha (Golden na Glitter).


Na Hastin Liumba, KigomaGOMBE ni kati ya Hifadhi za taifa zilizopo nchini ambapo ni sehemu ambayo watalii wengi wa ndani na nje wamekuwa wakiitembelea na kuliingizia taifa fedha za kigeni.
Muongozaji wageni katika hifadhi hiyo Hussein Halid Kengwa aliongoza jopo la waandishi waliotembelea Hifadhi ya Taifa Gombe na kujionea aina mbalimbali za wanyama ndani ya hifadhi.
Anataja aina za wanyama walioko ndani ya hifadhi hiyo ni Sokwe Mtu,nyani, nyani wa kijivu, kima wa mkia wa blue, mwenye mkia mwekundu na Chotara, Mbega mwekundu, Pongo na Nguruwe pori na aina mbali za nyoka na jamii ya Chatu.
Hussein anataja baadhi ya aina za nyoka wanaopatikana kwenye hifadhi ya Taifa Gombe ni Green Mamba, Black Mamba (Koboko),Gatigati Viper (Kilamata),Kobra,Python (Chatu).
Alitaja wanyama wengine ni Kakakuona,Nsha,Nungunungu,Mhanga na Civet (Paka Mwitu).
Aidha Hussein anasema wanyama hawa wengine wanakula matunda aina ya Budiamkonde,michikichi  na wngine hula nyama hususani Sokwe na Nyani hula nyama za Nguruwe Pori.
Aidha chakula kigine wanachokula Sokwe ni matunda ya miti iitwayo michikichi.
Anasema kwa upande wa Nyani licha ya kula matunda pia hula Nyama na mara nyingine hupenda kusogelea watalii na anapoona umeshika mkate anaweza kukupokonya kwani hupenda sana.

Maradhi yanayosumbua Sokwe na Nyani
Anasema maradhi ambayo yamekuwa yakisumbua wanyama hao ni magonjwa hasa Polio na mafua, homa ya mapafu.
Anasema licha Ferdinand kuwa kiongozi kuna Sokwe wengine waitwao Gaya na Gremli.
Akizungumzia maisha ya Sokwe anasema huishi kama familia katika Hifadhi hiyo na kwamba kiongozi wao mkuu huitwa Ferdinand.
Anabainisha Sokwe hakika hupanga uzao kama binadamu tena yawekana Sokwe wakawa wazuri kwenye eneo hilo kwani wanazaa kila baada ya miaka minne.
Hussein aliongeza kuwa Sokwe anapozaa hunyonyesha kwa muda wa miezi sita na baada ya hapo huanza kumtafutia mtoto wake chakula kama matunda na vinginevyo.
Anasema Sokwe wako makundi mawili kwenye hifadhi hiyo lakini kiongozi yupo mmoja ambaye ni Ferdinand.
Aidha aliongeza kuwa Sokwemtu wapatao 110 nyingine ni Mahale ikiwa na Sokwemtu wapatao 800, na Rubondo Sokwemtu wapo 30.
Hussein anabainisha Sokwe mtu licha kuwa na uongozi kwenye maisha ya familia zao bado huwa hawapende watalii kutowatii.
Anasema Sokwe unapokutana naye njiani unapaswa umpishe kwani usipompisha unapigwa na hilo anafanya akihisi unataka kuchukua utawala wao kwenye makazi yao.
Hatua nyingine mtalii anapokutana na kundi la Sokwe ili kuonyesha unawamtii unakumbatia mti ama mnakumbatiana mkiwa mmeinama.
Aidha anasemaSokwe sifa nyingine waliyonayo huweka ulinzi na kukagua mipaka yao kwenye maeneo wanayoishi.


Maporomoko ya maji Kakombe
Anasema ndani ya hifadhi hiyo  kuna vyanzo vingi vya maji vinavyotokea Hifadhini na kumwaga maji Ziwa Tanganyika yakiwemo maporomoko ya kuvutia ya Kakombe na Mkenke.
Anema maporomoko hayo ndipo mwanamuziki Diamond alitengeneza filamu yake ya wimbo wa Leka Dutigite.
Muongoza wageni huyo anaongeza maporomoko hayo wakazi wa vijiji vipatavyo vitano vikiwemo Mwamgongo, Mtanga, Mgaraganza, Bubango na Chankele zamani walikuwa wakitumia maporomoko hayo kufanyika matambiko
yao.

Maisha ya Nyoka ndani ya hifadhi
Hussein anaeleza ndani ya hifadhi kuna zaidi ya Nyoka 20 na nyoka hao hula wadudu kama mijusi, panya na mara nyingi hutembea sana nyakati za usiku.
Aidha Nyoka hao wanapotembea nyakati za usiku ni hatari kwao kwani mara nyingi Nyoka huuma usiku kuliko nyakati za mchana.
Kwa upande wa Chatu wapo wengi na wakubwa hawa huwinda mnyama aina ya mbuzi aitwaye Nsha na mara kadhaa hukamata hata Nyani. 
Aidha hukamata Nyani endapo anakuwa pekee kwani wwapo makundi Chatu huwa hathubutu kwani wana uwezo mkubwa wa kumshambulia.
Kuhusu Kakakuona,Pongo na Nsha anasema hawa wana eneo lao ambalo hupendele kukaa.
Aidha anasema hifadhi ya taifa Gombe imedumu kama makazi ya asili ya kudumu ya wanyama kwa sababu ni sehemu ndogo iliyojitenga na Ikolojia yake imezungukwa na mipaka ya asili.

Changamoto za eneo la hifadhi
Changamoto niliyoiona ndani na nje ya hifadhi baada ya kutembelea hifadhi ya Taifa Gombe ni mawasilino ya simu za kiganjani.
Eneo hilo halina mnara wa maawasilino ya simu kwani hakuna mnara wa Vodacom,Airtel na Tigo ambapo watumishi wa hifadhi hiyo hutegemea kupiga simu kwa kutegea sehemu moja ilikudaka mawimbi ya kutoka kijiji cha Mwamgongo.

Wakazi kijiji cha Mwamgongo wanufaika na hifadhi hiyoWakazi wa kijiji jirani cha Mwamgongo wamesema wananufaika zaidi na hifadhi hiyo katika eneo la mahitaji ya kijmii.
Mtendaji wa kijiji cha Mwamgongo Hussein Omari alisema hifadhi ya taifa ya Gombe imekuwa mkombozi kwani kwa kutoa msaada mbalimbali.
Alisem misaada hiyo hifadhi kuwajengea nyumba mbili za walimu shule za msingi na sekondari,darasa moja na kwamba kijiji hicho kina kaya 860 zenye wakazi 5,550.

hastinliumba@gmail.com-0788390788

No comments:

Post a Comment