Washtakiwa Mathew Jeremia, Paschal Mashiku Lugoye, Alex Joseph Bugwema Silola Jangalu na Chacha Jeremia wakiingia mahakama jana tayari kuanza kusikilizwa kwa kesi dhidi yao. (PICHA NA DANIEL MBEGA).
Na Daniel Mbega, Mwanza
SHAHIDI wa
sita katika kesi ya mauaji ya Aaron Nongo mwenye ulemavu wa ngozi (albino),
Mkaguzi wa Polisi (Inspector) David Mhanaya, ameanza kutoa ushahidi wake leo
hii katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza.
Mbele ya
Jaji Robert Makaramba anayesikiliza Shauri hilo namba 213 la mwaka 2014,
shahidi huyo ametumia siku nzima kutoa ushahidi wake akiongozwa na mawakili wa
serikali Emil Kiria, Esther Majaliwa na Robert Kilando.
Hata hivyo,
Jaji Makaramba aliahirisha kesi hiyo hadi keshokutwa Mei 14, 2015 baada ya
kutokea mgongano wa kisheria katika masuala ya vidhibiti kufuatia pingamizi la
Wakili Makwega wa upande wa utetezi, hivyo siku hiyo atatoa uamuzi kuhusiana na
pingamizi hilo.
Washtakiwa
katika kesi hiyo ni Chacha Jeremia, Mathew Jeremia Mlimi, Paschal Lugoye
Mashiku na Alex Joseph maarufu kama Bugwema Silola Jangalu.
Marehemu Nongo
aliuawa Juni 26, 2009 majira ya saa tatu usiku akiwa nyumbani kwake Ibanda
Relini, jijini Mwanza ambapo wauaji hao walimkata usoni na kisha kumkata miguu
yake yote miwili na kutoweka nayo pamoja na meno mawili ya mbele.

No comments:
Post a Comment