Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 12 May 2015

WATUHUMIWA 12 WAGOMA KUINGIA MAHAKAMANI


Na Hastin Liumba, Nzega
LICHA ya Agizo la Jaji Mkuu Othumani Chande kuzitaka mahakama kushughulikia Tatizo la Mlundikano wa kesi mahakamani, kumekuwa na tatizo la kupigwa danadana  baadhi ya kesi hapa nchini  na kusababisha malalamiko kwa wafungwa.


Wakizungumza 
na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti baadhi ya wafungwa wamekiita kitendo hicho ni cha makusudi kinachofanywa na baadhi ya wanasheria wa serikali wanaosimamia kesi hizo.

Wakizungumzia kesi ya jinai Namba 83 ya mwaka 2009 ya Unyang'anyi wa kutumia silaha katika mgodi wa dhahabu wa Resolute walisema kuwa kesi hiyo ina miaka saba hadi sasa bado inasikilizwa hali ambayo imekuwa ni kero kwa wana ndugu wa mahabusu.

Aidha wametoa rai kuutaka muhimiri huo muhimu wa Dola ambao unaaminika na jamii  kusikiliza haraka kesi hiyo ya zamani na kuzitolea hukumu ilikutoa haki kwa Watanzania.

Watuhumiwa 12 wa kesi hiyo ya unyanganyi wa kutumia silaha katika mgodi wa dhahabu wa resolute jana waligoma kushuka katika gari la polis kuingia katika mahakama ya hakim mkazi wilaya ili kesi hiyo isomwe.

Wakizungumza wakiwa wamekaa ndani ya gari la polisi wameutupia lawama upande wa Jamuhuri kwa kuchelewesha kesi yao kwa muda mrefu hali ambayo imekuwa kero kwao na kwafamilia zao.

Edward Bunela mmoja ya watuhumiwa wa kesi hiyo akizungumza kwa uchungu alisema mahakama inapaswa kuwatendea haki kutokana na kuhudhuria kila siku mahakamani hapo bila mafaniko kwa muda wa miaka saba hadi sasa.

Alimuomba Jaji mkuu Otuhumani Chande kuingilia kati shitaka hilo ili hatua iliyosalia iweze kukamilika kwa muda stahiki na kuongeza kuwa baadhi ya  wanasheria wa Jamuhuri wamekuwa wakitoa tambo mbalimbali kwa watuhumiwa hao.

‘’Tunamuomba Jaji mkuu aingilie kati miaka saba mpka sasa tunapigwa danadana upande wa jamhuri unatusumbua wanafanya tekinik za kuchelewesha kesi sisi tunataabika gerezani ni bora hukumu itoke tujue hatima yetu’’alisema Edward.

Shaabani Amour mshitakiwa alisema kuwa hawajui hatima yao kutokana na kutojulikana mwenendo wa kesi yao na kuziomba mamlaka za juu kuwasaidia ili kutekeleza agizo la Jaji Mkuu.

Hakim mkazi wa mahakama ambaye ansikilizi kesi hiyo Spraphine  Nsana alisema kuwa tatizo ni wakili wa washitakiwa namba 14,15 na 16 ana kesi katika mahakama ya Rufaa hivyo hakuweza kuhudhuria shauri hilo.

Alisema kuwa wakili huyo wa watuhumiwa watatu aliwasilisha barua ya taarifa katika mahakama hiyo na kuongeza kuwa siku hiyo ilikuwa ni kusomwa kwa kesi hadi hapo may 25 mwaka huu itakapo somwa tena.

Baadhi ya ndugu wa watuhumiwa hao wameutupia lawama upande wa Jamuhuri kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake kutokana na kesi hiyo kuchukua muda mrefu huku hakuna kinachoendelea.

Hivi karibu jaji mkuu wa Tanzania Otuhumani Chande alipofanya ziaza ya kikazi mkoani hapa  waliwataka mahakimu wa mahakama za mwanzo, wilaya ,mkoa na mahakama kuu kuhakikisha wananmaliza kesi ambazo zina miaka saba hadi miwili ilii kupunguza msongamano katika mahabusu za mkoa wa Tabora

Licha ya kupunguza kesi hizo ambapo kila hakimu anatakiwa kumaliza kesi 260 ili kwenda na kasi ya kupunguza msongamano kwenye magereza ya mkoa na nchi kwa ujumla wake .

Hata hivyo alizitaka taasisi hiyo kupunguza urasimu wakati wa usikilizwaji na kutoa uhamuzi wa  kesi mbalimbali katika mahakama hizo.

No comments:

Post a Comment