Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akizungumza na wajumbe
wa Bodi ya Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) mjini Moshi. Katika hotuba
yake Rwegasira aliitaka Bodi hiyo ifanye kazi kwa ushirikiano kwa maendeleo ya
chuo. Wapili kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli.
Kushoto ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, na Mwenyekiti
wa Bodi ya Chuo, Kinemo Kihomano. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Kaimu Kamishna Jenerali wa
Uhamiaji, Victoria Lembeli akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Chuo cha Uhamiaji
cha Kikanda (TRITA) katika hafla fupi ya uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika
mjini Moshi. Watatu kulia meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira. Kushoto ni Kamishna wa Uhamiaji
Zanzibar, Johari Masoud Sururu, wapili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo, Kinemo
Kihomano.na kulia ni Kamishna wa Chuo hicho, John Choma.
Mkufunzi Mkuu wa Chuo cha
Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) mjini Moshi, Erasmi Francis akimuonyesha Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kushoto)
na wajumbe wa Bodi ya Chuo hicho, kamera inayotumika kuchukua kumbukumbu za
usalama kwa ajili ya watu wanaopita katika mipaka ya nchi. Wapili kushoto ni
Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli. Watatu kulia ni Kamishna
wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo
hicho, Kinemo Kihomano (Wasita kushoto).
Mkaguzi wa Uhamiaji ambaye
pia ni Mkuu wa Kitengo cha Tehama, Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) mjini
Moshi, Zawad Chazuka akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati) albamu yenye hati za kusafiria
za mataifa mbalimbali duniani, albamu hiyo inaonyesha alama za kiusalama ambazo
zipo katika pasipoti za mataifa mbalimbali. Kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali
wa Uhamiaji, Victoria Lembeli.
Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo
cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) mjini Moshi, Kinemo Kihomano, akizungumza na
wajumbe wa bodi (hawapo pichani, mara baada ya bodi hiyo kuzinduliwa na Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira
(katikati). Kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli.
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kushoto) akimsalimia
Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli, wakati alipokuwa
anawasili katika Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) mjini Moshi kwa ajili ya
kuzindua Bodi ya Chuo hicho. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akikagua maeneo
mbalimbali ya Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) mjini Moshi. (kushoto) mara
baada ya kuzindua Bodi ya Chuo hicho. Katikati ni Kaimu Kamishna Jenerali wa
Uhamiaji, Victoria Lembeli, na kulia ni Kamishna wa Chuo hicho, John Choma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati waliokaa), Kaimu
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli (wapili kushoto waliokaa),
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu (kushoto) wakiwa katika
picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA),
mara baada ya Katibu Mkuu huyo kuzindua Bodi hiyo mjini Moshi. Picha
zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment