Alex Msama
Na Mwandishi Wetu
KAMATI ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka 2016 limeutangaza mkoa wa Geita kuanza na Tamasha la Pasaka mwaka huu kabla ya Mwanza.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi, Alex Msama Machi 27, tamasha litahamia jijini Mwanza.
Msama alisema Kamati yake bado inaendelea na mchakato wa kufanikisha tamasha la Pasaka ambalo mwaka huu litakuwa na miaka iliyopita.
“Geita ni mkoa ambao ulionesha kulihitaji Tamasha la Pasaka kama ilivyokuwa Mwanza ndipo tulipoona kwamba tuanze na mkoa huo kwani maombi yalikuwa ni mengi zaidi,” alisema Msama.
Aidha Msama alisema wamesikia kilio cha wakazi wa Geita baada ya maombi yao ya muda mrefu, tamasha litafanyikia mkoani humo ikiwa ni heshima yao.
“Wakazi wa Geita walipokee kwani litashirikisha idadi kubwa ya waimbaji wa ndani ni shereje, raha, vifijo,” alisema Msama.
No comments:
Post a Comment