Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday, 17 July 2015

WANACHAMA 12 WACHUKUA FOMU ZA UBUNGE NZEGA

Hussein Bashe (kushoto) akiteta jambo la Mbunge wa sasa wa Nzega Mjini, Dk. Hamisi Kigwangallah.

Na Hastin Liumba, NzegaKADA wa chama cha mapinduzi (CCM) Joseph Ngulumwa ameishauri serikali kuingalia upya sheria ya madini kwa wachimbaji wadogo ya mwaka 2010 ili iweze kunufaisha kundi hilo.

Hayo aliyasema mara baada ya kuchukua fomu ya kuwani ubunge jimbo la Nzega mjini wakati akiongea na waandishi wa habari.
Ngulumwa ambaye ni mtaalamu wa miamba na madini (Mjiolojia-Shahada ya kwanza ya madini), alisema endapo sheria hiyo litafanyiwa marekebisho kundi la wachimbaji wadogo litanufaika na mikopo toka taasisi mbalimbali za fedha.
Alisema endapo atapewa ridhaa ya kuliongoza jimbo la Nzega mjini vipaumbele vyake itakuwa ni elimu, Maji, michezo, Barabara, Madini, Ardhi na Afya.
Ngurumwa alisema ana uzoefu mkubwa ndani ya CCM kwa miaka 25 hivyo haoni jambo gumu kwake kuwania ubunge.
Alisema anaomba nafasi ya ubunge ili aweze kusadia watu na siyo vinginevyo na kudai anatosha katika nafasi hiyo.
Hadi sasa tayari wanachama 12 wamejitokeza kuchukua fomu za kuwania ubunge katika majimbo ya Nzega mjini,Bukene na Nzega vijijini.
Wanachama hao ni Joseph Ngulumwa (Nzega mjini), Hussein Bashe (Nzega Mjini).
Jimbo la Bukene ni Suleiman Zedi,Teddy Kasela Bantu, Charles Mazigwa, Deogratias Kahumbi, kati ya hao wawili Yasin Memba na Laurant Shauri tayari wamerejesha fomu zao.
Katibu wa CCM wilaya ya Nzega Epimark Makuya  alisema mwisho wa kurejehsa fomu ni mwezi Julai 19 mwaka huu saa 10:00 jioni na akawataka wanachama hao kuziingatia masharti na kanuni za chama ikiwemo kutofanya kampeni kabla ya muda.

No comments:

Post a Comment