Taifa Stars inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premieum Lager leo Jumamosi saa 10 kamili kwa saa za Afrika Mashariki itashuka dimba la Nakivubo kucheza na wenyeji Uganda.(The Cranes).
Mecho hiyo ya leo ni ya marudiano kuwania kufuzu kwa fainali za CHAN mwaka 2016 zitakazofanyika mapema mwezi Januari nchini Rwanda, mgeni rasmi atakua Rais wa Uganda Yoweri Mseveni.
Kikosi cha Taifa Stars chini ya kocha wake mkuu Charles Mkwasa, kiliwasili jijini Kampala juzi usiku na kimefikia katika hoteli ya Grand Global iliyopo jirani na chuo kikuu cha Uganda Makerere.
Taifa Stars imefanya mazoezi jana jioni katika Uwanja wa Nakivubo yakiwa ni mazoezi mepesi na mwisho kuzoea uwanja kabla ya mchezo wenyewe utakaofnayika leo jioni.
Kocha Mkwasa akiongelea kuelekea mchezo huo amesema, anashukuru vijana wake wamefika salama wote, hali zao ni nzuri, morali ni ya hali ya juu, kikubwa wanatambua wana deni kubwa kwa watanzania hivyo leo watapambana kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.
Akiongelea hali ya hewa na mazingira ya timu ilipofikia, Mkwasa amesema hali ya hewa ni ya kawaida baridi na mvua kidogo haina tofauti sana na Tanzania, mazingira ya hoteli ni mazuri na kusema kikubwa kilichobaki ni kusaka ushindi katika mchezo huo na vijana wake wapo tayari.
Wakati huo huo, mashabiki zaidi ya 50 kutoka nchini Tanzania wanatarajiwa kuwasili kesho jumamosi alfajiri wakitokea jijini Dar es salaam kuungana na watanzania wengine waishio nchini Uganda kuishangilia timu ya Tanzania itakapokuwa ikipimbana na Uganda katika uwanja wa Nakivubo.
No comments:
Post a Comment