Kikosi cha Simba SC ambacho mwaka 1995 kilitwaa ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati kwa mara ya nne jijini Dar es Salaam. Waliosimama kutoka kushoto ni aliyekuwa mfadhili mkuu wa klabu hiyo Azim Dewji, Madaraka Kibode Selemani 'Mzee wa Kiminyio', Godwin Aswile Mlimba 'Scania', Mohammed Mwameja, Hussein Marsha 'Smart Boy', Mustafa Hoza na George Magere Masatu.
Walioinama mstari wa mbele ni Athumani Abdallah China 'Injini', Dua Said, Deo Mkuki, Idd Kibode Selemani 'Meya' na Edward Cyryl Chumila.
Na Daniel Mbega wa brotherdanny.com
‘WANYAMA wa Msimbazi’
Simba SC ya Tanzania wana rekodi ya pekee katika mashindano ya Klabu Bingwa
Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame, ikiwa ndiyo klabu
iliyocheza mechi nyingi zaidi na kutwaa ubingwa mara nyingi pia tangu
mashindano hayo yalipoanza rasmi mwaka 1974.
Utafiti uliofanywa na brotherdanny.com unaonyesha pia kwamba, katika
kipindi cha miaka 40 ya mashindano hayo, jumla ya mechi 745 zimechezwa huku
zikizaa mabao 1776, ukiwa ni wastani wa mabao 2.3 kwa kila mechi.
Kwa kuangalia rekodi hizo, Simba SC, ambayo mwaka huu haimo kwenye
kinyang’anyiro cha michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Julai 18 jijini Dar es
Salaam, inaongoza kwa kutwaa taji hilo mara sita (6) ikifuatiwa na Yanga ya
Tanzania, AFC Leopards na Tusker FC za Kenya ambazo zimetwaa mara tano kila
moja.
Simba SC ilitwaa ubingwa huo katika miaka ya 1974, 1991, 1992, 1995,
1996 na 2002; Yanga (1975, 1993, 1999, 2011 na 2012); AFC Leopards ambayo
zamani ilijulikana kama Abaluhya (1979, 1982, 1983, 1984 na 1997); na Tusker FC
zamani ikijulikana kama Kenya Breweries (1988, 1989, 2000, 2001 na 2008).
Klabu za APR ya Rwanda, Gor Mahia ya Kenya, El-Merreikh ya Sudan na SC
Villa ya Uganda zimetwaa taji hilo mara tatu kila moja, wakati ambapo Luo Union
ya Kenya imetwaa mara mbili na ndiyo klabu ya kwanza kutwaa taji hilo mfululizo
katika miaka ya 1976 na 1977.
Klabu zilizotwaa mara moja ubingwa huo ni Atraco na Rayon Sports za
Rwanda, Kampala City Council na Polisi FC za Uganda na Vital’O ya Burundi.
Kenya ndiyo inayoongozwa kwa klabu zake
kutwaa ubingwa mara nyingi zaidi, ambapo kwa jumla zimetwaa mara 15, Tanzania imetwaa
mara 11, Rwanda na Uganda mara 5 kila moja, Sudan mara tatu na Burundi mara
moja.
Hata hivyo, Simba SC inaongoza pia kwa
kucheza fainali 9, ikifuatiwa na Yanga, APR na AFC Leopards zilizocheza fainali
8, El-Merreikh na Tusker FC (6), SC Villa (5), Gor Mahia (4), Luo Union, KCC,
Express FC na URA (2).
Kwa ujumla, timu 129 zimeshiriki mashindano hayo ambayo hayakupata kufanyika mwaka 1990.
Kwa upande mwingine, Simba SC kwa kucheza
jumla ya mechi 101 kwenye michuano hiyo, ikiwa imeshiriki mara 23. Katika mechi
hizo, imeshinda 54, imetoka sare 17 na kufungwa 30, wakati ambapo imepachika
jumla ya mabao 138 na kufungwa 77.
Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga wanashika
nafasi ya pili kwa kucheza mechi 84, wakishinda 45, sare 14 na kupoteza 25,
wakati imefunga mabao 121 na kufungwa 89.
APR ndiyo ya tatu kwa kucheza mechi 75,
kushinda 40, sare 12 na kufungwa mechi 18 huku ikipachika mabao 133 na kufungwa
69.
Sports Club Villa yenyewe inashika nafasi
ya nne kwa kucheza mechi 77, kushinda 42, sare 12 na kupoteza 23 lakini
ikitikisa nyavu mara 118 na kufungwa 60.
AFC Leopards, ambayo ndiyo timu pekee
kubeba kombe moja kwa moja baada ya kushinda mara tatu mfululizo katika miaka
ya 1982, 1983 na 1984, inashika nafasi ya tano kwa
kucheza mechi 59, kushinda 38, sare 8 na kupoteza 13, huku ikipachika mabao 80
na kufungwa 43.
Nafasi ya sita inashikwa na El-Merreikh kutoka
Omdurman nchini Sudan, ambayo imecheza jumla ya mechi 45, kushinda 28, sare 10
na kufungwa mechi 7, lakini ikitikisa nyavu za wapinzani mara 67 na kuruhusu
wavu wake utikiswe mara 27.
Tusker FC yenyewe imecheza mechi 50, kushinda 27,
sare 10 na kupoteza 13, na ikafunga jumla ya mabao 74 na kufungwa 31.
Gor
Mahia, timu pekee ya Afrika Mashariki kutwaa Kombe la Washindi Afrika, ambalo
sasa limefutwa, inashika nafasi ya nane kwa kushinda mechi 24 kati ya 54
ilizocheza, kutoka sare 15 na kupoteza 16, lakini ikifunga jumla ya mabao 75 na
kufungwa 49.
Kampala
City Council imecheza mechi 38, imeshinda 19, sare 5 na kufungwa 14, ikifunga
mabao 48 na kufungwa 39, wakati ambapo nafasi ya kumi inashikwa na Express FC
ambayo nayo imecheza mechi 38, lakini imeshinda 17, sare 4 na kufungwa 17, huku
ikipachika mabao 55 na kufungwa 42.
Huu ndio msimamo wa miaka yote wa michuano ya
Kagame:
1.Simba
SC 101 54 17 30 138-
77 179 [Tanzania]
2.Yanga 84
45 14 25 121- 89 149 [Tanzania]
3.APR
FC 75 40
12 18
133- 69 147 [Rwanda]
4.SC
Villa 77 42 12
23 118- 60 137
[Uganda]
5.Abaluhya
FC 59 38 8 13 80- 43 122 [Kenya]
6.El
Merreikh 45 28
10 7 67- 27 94 [Sudan]
7.Breweries
(Tusker) 50 27
10 13 74- 31 91 [Kenya]
8.Gor
Mahia 54 24 15
16 75- 49
87 [Kenya]
9.Kampala
CC 38
19 5 14 48- 39 62 [Uganda]
10.Express
FC 38 17 4 17 55- 42 55 [Uganda]
11.Saint
George 32 16 6
10 64- 26 54
[Ethiopia]
12.Al
Hilal 38 13 9
16 42-41 48 [Sudan]
13.Vital’O 33 13 5 14
48- 43 47 [Burundi]
14.Rayon 31 13 5 15
56- 49 44 [Rwanda]
15.URA 21 11 2 8 36- 26
35 (Uganda)
16.Ulinzi
Stars 21 9 4 8 34-
30 31 (Kenya)
17.Luo
Union 13 9 1
3 24- 13
28 [Kenya]
18.Limble
Leaf Wd. 17
8 4 5 19- 17 28 [Malawi]
19.Navy
FC (KMKM) 33 7 5
21 20- 52 26
[Zanzibar]
20.ATRACO 16 8 0
8 27-
25 24 (Rwanda)
21.Bata
Bullets 21 6 4
10 19- 26 22
[Malawi]
22.Police
FC 10 6 0
4 15-
13 18 (Uganda)
23.Horsed 16 4 6 6 12- 17 18 [Somalia]
24. Atletico Olympique 13 5 2 6 14- 14 17 (Burundi)
25.El
Mourada 11 3 4
4 7- 10 16
[Sudan]
26.Azam 10 4 4
2 15-
8 16 (Tanzania)
27.Red
Sea 13 5 1
7 16- 19 16 [Eritrea]
28.Police 6 5
0 1 8-
3 15 (Rwanda)
29.Sofapaka 6 5 0 1 9-
2 15 (Kenya)
30.Oserian 9 4 2 3 11- 7 14
[Kenya]
31.Coastal
Union 8 4 2 2
5- 6 14
[Tanzania]
32.Green
Buffaloes 8 4 1 3 13- 9 13 [Zambia]
33.Mufulira
Wand. 12
3 4 5
8- 7 13 [Zambia]
34.Small
Simba 23 2 7
14 11- 27 13
[Zanzibar]
35.Elman 27 2 7 18
14-48 13
[Somalia]
36.Muzinga 10 4 1 5
22- 15 13 [Burundi]
37.TP
Mazembe 6 4
0 2
22- 7 12 (Congo-Kinshasa)
38.Moro
United 6 4
0 2 13-
6 12 (Tanzania)
39.
Kiyovu Sport 6
3 2 1 16-
10 11 (Rwanda)
40.Prince
Louis 6 3 1 2
9- 5 10
[Burundi]
41.Rio
Tinto 9 2 4
3 10- 11 10 [Zimbabwe]
42.Mlandege 12 2 4 6
9- 15 10 [Zanzibar]
43.AS Vita
Club 6 3
1 2 14-
8 10 (Congo-Kinshasa)
44.Zimbabwe
Saints 5 3 0 2
5- 4 9 [Zimbabwe]
45.Mathare
United 6 3
0 3 7-
7 9 (Kenya)
46.Express
FC 10 2 3 5
9- 19 9 [Uganda]
47.Mtibwa
Sugar 9 2 3 4 10- 14 9
[Tanzania]
48.ADMARC
Tigers 5 2 2 1
6- 5 8 [Malawi]
49.Silver
Strikers 4 1 2 1
5- 6 8 [Malawi]
50.Mebrat
Hail-EELPA 10 0 8 2 8-
13 8 [Ethiopia]
51.Merreikh
(Al-Fasher) 6 2 1
3 7-
5 7
(Sudan)
62.Miembeni 9 2 1 6 4- 19 7 [Zanzibar]
63.Mukura
Victory 5 2 1 2
10- 9 7
[Rwanda]
64.Berec
Power Pk. 6 2 1 3
2- 4 7 [Malawi]
65.Simba
FC 7 1 3
3 7- 9 6
[Uganda]
66.JS
St.Pierroise 3 2 0 1
6- 2 6 [Reunion]
67.Nzoia
Sugar 4 2 0
2 11- 8 6 [Kenya]
68.Maji
Maji 4 2 0
2 3- 4 6 [Tanzania]
69.CDE/CDA 7 2 0 5 5-
21 6
[Djibouti]
70.Awassa Kenema 6 1 3 2 5- 7 6 (Ethiopia)
71.Ocean
View 4 2
0 2 5-
4 6 (Zanzibar)
72.Nkana
Red Dev. 4 1 2 1
4- 3 5 [Zambia]
73.Khartoum
3 5 1 2
2- 4 5
[Sudan]
74.Hay al-Arab 4 1 2 1 5-
8 5 (Sudan)
75.Bunamwaya 4 1 1 2 8-
6 4 (Uganda)
76.AS
Port 10
1 1 8 5-44 4 (Djibouti)
77.Al-Ahli
(Shandi) 3 1
1 1 3-
3 4 (Sudan)
78.AS Ali
Sabieh/Dj.Tél. 4 1 1 2 5-
6 4 (Djibouti)
79.Inter
Star 4 1
1 2 4-
6 4 (Burundi)
80.Banaadir
Telecom 9 1 1
7 8-38 4 (Somalia)
81.Pan
African 3 1 1
1 6- 3 4
[Tanzania]
82.Kiyovu
Sport 3 1 1 1 3-
3 4
[Rwanda]
83.Blue
Bats 3 1 1
1 1- 2 4
[Uganda]
84.Morris
Supplies 3 1 1 1 3-
4 4 [Somalia]
85.MDC
United 3 1 1 1 2-
3 4 [Malawi]
86.Nkana
Red Dev. 4 1 1
2 4-
5 4 [Zambia]
87.Jeshi 5 0 4 1 2-
3 4 [Zanzibar]
88.MBC
Munic’lity 7 1 1 5 3-
13 4 [Somalia]
89.Mseto
Sports 4 1 1 2 5-
10 4 [Tanzania]
90.Kabwe
Warriors 4 1 0
3 5- 8 3
[Zambia]
91.Breweries 3 1 0 2 1-
3 3 [Uganda]
92.Red
Arrows 4 1 0
3 6- 7 3
[Zambia]
93.Civo
United 4 1 0
3 3- 6 3 [Malawi]
94.Nchanga
Rangers 3 1 0 2 3-
3 3 [Zambia]
95.Malindi 8 0 3 5 5-
12 3 [Zanzibar]
96.Ujamaa 3 1 0 2 3- 7 3 [Zanzibar]
97.Inter
Stars 4 1
0 3 3-
4 3 (Burundi)
98.Atlabara 5 0 3 2 5-
8 3 (South Sudan)
99.Printing
Club 4 0 2 2 6-10
2 [Somalia]
100.Adama
City 4 0
2 2 4-
8 2 (Ethiopia)
101.Mafunzo 5 0 2 3 2-
10 2 (Zanzibar)
102.Elect-Sport 3 0 2 1 5-
7 2 (Chad)
103.Al-Hilal
(Kaduqli) 2 0 1
1 1-
2 1 (Sudan)
104.Rangers
FC 3 0 1 2 1- 4 1 [Malawi]
105.Tukuyu
Stars 4 0 1 3 4-10
1 [Tanzania]
106.Petroleum
Agcy. 4 0 1 3 2-12
1 [Somalia]
107.East
Coast 2 0 1
1 1- 3 1 [Somalia]
108.Information
C. 3 0 1 2 1- 4 1 [Somalia]
109.Tornados 3 0 1 2 2- 7 1 [Zimbabwe]
110.Prisons 3 0 1 2 3-
8 1 (Tanzania)
111.Adulis 5 0 1 4 3- 10 1 [Eritrea]
112.
Jamhuri 4 0 1
3 5-17 1 (Zanzibar)
113.Gendarmerie
N. 4 0 0
4 1-25 0
(Djibouti)
114.Hardware
Stars 2 0 0 1 1- 4 0 [Malawi]
115.Uganda
Com. Bk. 3 0 0 3 1- 5 0
116.Forodha 4 0 0 4 2- 9 0
[Zanzibar]
117.Naadiga
Dek. 2 0 0 2 2-10 0
[Somalia]
118.Wagad 4 0 0 4 2-11 0 [Somalia]
119.Alba 3 0 0 3 1-11 0 [Somalia]
120.Marine 4 0 0 4 0-14 0 [Somalia]
121.Telecoms 3 0 0 3 1-15 0
[Ethiopia]
122.Borrer 3 0 0 3 1-18 0
[Djibouti]
123.Djibouti
Telecom 2 0 0
2 2-
9 0 (Djibouti)
124.Kartileh
DjibSat 3 0 0
3 1-14 0 (Djibouti)
125.Polisi 7 0
0 7 2-
12 0 (Zanzibar)
126.SID 4 0
0 4 3-19 0 (Djibouti)
127.Al-Tahrir 3 0 0 3 5-
8 0 (Eritrea)
128.Etincelles 4 0 0 4 4-12 0 (Rwanda)
129.Al-Salaam
(Wau) 3 0 0
3 1-19 0 (South Sudan)
IMEANDALIWA NA www.brotherdanny.com (Unapoitumia makala hii tafadhali rejea chanzo)
No comments:
Post a Comment