Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday, 11 May 2015

MWANDISHI AKANUSHA MADAI YA MAREKANI KUHUSU MAUAJI YA OSAMA BIN LADEN

Obama akitizama operesheni iliyomuua Osama bin Laden
Mwaandishi mmoja mashuhuri kwa ripoti za upekuzi, Seymour Hersh, amekanusha madai ya utawala wa Rais Obama kuhusiana na kuuawa kwa kinara mkuu wa kundi la wapiganaji la Al-Qaeda, Osama Bin Laden, nchini Pakistan miaka 8 iliyopita.

Akiandika katika jarida la London Review of Books, Bwana Hersh, alikanusha madai ya Washington kuwa, kutekwa na kisha kuuawa kwa kiongozi huyo wa AlQaeda ilikuwa ni janja janja za shirika la kijasusi la Marekani CIA.
Hersh anasema ukweli ni kuwa walisaidiwa pakubwa na shirika la kijasusi la Pakistani.
Aidha kiongozi mkuu wa kijasusi wa Pakistan anasemekana kuongoza mikakati ya operesheni hiyo ya kisiri.
Mwaandishi mmoja amekanusha madai ya utawala wa Rais Obama kuhusiana na kuuawa Osama Bin Laden
Wakati ambapo Pakistan ilipojitenga na uvamizi huo na kuutaja kama ukiukaji wa uhuru na mipaka yake.
Marekani wala Pakistan hazijasema chochote hadi kufikia sasa.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment