Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 12 May 2015

FRANK KIBIKI AHIMIZA VIJANA KUJIUNGA NA VIKOBA

Na Mwandishi Wetu, Iringa
VIJANA Manispaa ya Iringa,  wametakiwa kujiunga kwenye vikundi vya ujasiriamali na kutumia  fursa zilizopo kwenye  maeneo yao ili waweze kujiajiri na hivyo kujikwamua na hali ngumu ya maisha.

Wito huo umetolewa na mwanahabari Frank Kibiki, wakati akizungumza na vijana waliojiunga kwenye Kikundi cha Tujiwezeshe Vikoba cha stendi kuu ya mabasi ya mjini Iringa, kilicho na wanachama 560.
Kibiki alisema, umoja ni nguvu na ikiwa vijana watajiunga kwenye vikundi hivyo vya kiujasiriamali itakuwa rahisi kufanikiwa kiuchumi.
“Tukiungana pamoja ni rahisi kufanikiwa kiuchumi, hakuna njia njia nyingine kwa sababu dhamana yetu vijana ni umoja tu, jiungeni kwenye vikundi vya ujasiriamali,”alisema Kibiki.
Alisema maeneo mengi ambayo vijana wameungana wameweza kukopeshwa, na wanaendesha shughuli zao za kiuchumi bila wasi wasi, jambo hilo linawezekana.
Katibu wa kikundi hicho cha Tujiwezeshe, Charles Manet alisema, waliamua kuungana baada ya vijana wengi wa maeneo hayo kukabiliwa na ugumu wa maisha.
Alisema mpaka sasa wanayo zaidi ya Sh Milioni 10, ambazo wamekuwa wakikopeshana kwa riba naafuu.
Alifafanua kuwa mara nyingi vijana wa stendi wamekuwa wakiachwa nyuma kwenye shughuli za kimaendeleo jambo ambalo, limewafanya waungane.
Walimtaka Kibiki ambaye hivi karibuni alitangaza nia ya kuwania nafasi ya Ubunge jimbo la Iringa mjini, kutokatishwa tamaa kutokana na mchango wake mzuri kwa kundi la vijana.
“Sisi tutaendelea kukuchangia na tupo pamoja na wewe Kibiki, kazi yako ya habari tunaikubali na kazi yako ya kutujali sisi tunaikubali, songa mbele kundi la vijana lipo nyuma yako,”alisema.

No comments:

Post a Comment