Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Wednesday, 13 May 2015
CHAWATIATA TABORA YATOA ONYO KALI KWA WAGANGA
Na Hastin Liumba, Tabora
WAGANGA wa tiba asilia mkoani Tabora wameonywa kutojihusisha na vitendo vyovyote vinavyochochea uvunjifu wa amani kwa kupiga ramli zinazoleta mauaji ya vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi (albino).
Mwenyekiti wa Chama Cha Waganga na tiba asilia (CHAWATIATA) Manispaa ya Tabora RamadhaniRajabu alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na gazeti hili kuhusu tuhuma zinazowakabili baadhi ya wananchama wake kujihusisha na vitendo hivyo viovu.
Alisema anaunga mkono kauli ya Serikali ya kuwakamata waganga wote wanaojihusisha na vitendo hivyo ikiwa ni pamoja na wale wanaotumia ramli chonganishi kwani wanaweza kuondoa amani ya nchi yetu ikiwa ni pamoja na kuwapa hofu ya kuishi wazee na albinism.
Alisema kila halmashauri ya wilaya mkoani humo inatakiwa kuwatambua waganga wa kienyeji waliopo na wenye vibali vya kufanya kazi hiyo kutoka kwenye chama na endapo mamlaka husika na kubainisha yule atakayebainika kwenda kinyume na masharti ya katiba ya chama hicho atachukuliwa hatua kali.
“Haiwezekani mganga anayetibu ama kutoa tiba ya kweli amshawishi mteja wake kuleta viuongo vya maalbino, huyo siyo mganga na hakuna tiba yoyote ya asili inayo tumia kiungo cha binadamu isipokuwa viungo vya baadhi ya wanyama ila sio binadamu,' alisema Rajabu.
Alisema inasikitisha sana kuona waganga wa tiba asili wakituhumiwa kuhusika na mauaji ya albino pamoja vikongwe jambo linawachafua hata waganga wengine ambao wanafuata maadili ya utoaji tiba hizo, na kuongeza kuwa hao ni matapeli na ni wenye tamaa ya fedha.
Aliitaka Jamii kutambua hakuna Mganga ambaye anaweza kumwagiza mteja wake kumletea kiungo cha albno ili kuweza kutibiwa kwani hata waganga wana watoto ambao ni albinism, ndugu zao
Aidha alisema Serikali inatakiwa kulitambua hili kama janga la kitaifa na siyo kwamba mauaji haya yanawahusu waganga wa kienyeji wote kama inavyoonekana bali inatakiwa kukaaa chini na kulitafutia ufumbuzi.
Hata hivyo aliomba wanachi kuungana kwa pamoja kuhakikisha ulinzi dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi unakuwepo na kutoa taarifa sehemu husika pale inapotokea albino au kikongwe kufanyiwa unyama wa aina yoyote ile ili kumaliza janga hili linalowakabili.
Aidha ameyataka medhehebu yote ya dini kuungana kwa pamoja kuliombea taifa juu ya janga hili la mauaji ya albino na vikongwe linalo zidi kushika kasi hapa nchini ikiwa ni pamoja taifa kupata sifa mbaya kwenye anga za kimataifa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment