Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 1 February 2016

WALEMAVU: MSAMA ANAJITAMBUA

Alex Msama

Na Mwandishi Wetu
BAADHI ya walemavu hapa nchini  wametoa wito kwa Watanzania wengine kujitambua kuhusu Mungu na mikakati mbalimbali ya kimaendeleo katika jamii ikiwa ni kuelekea Tamasha la Pasaka linalotarajia kufanyika Machi 27 jijini Mwanza.Akizungumza jana kwa niaba ya Esperance Wetewabo ambaye ni mlemavu wa mikono na mguu, mchungaji wa Godfrey Rubanzibwa 'Punda  wa Yesu' alisema jamii inatakiwa kujitambua kuhusu Mungu kama alivyo Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama anavyotekeleza majukumu yake katika muziki huo.
Punda wa Yesu alisema Msama amejitambua ndio maana anashirikisha kada mbalimbali katika jamii kuelekea Tamasha la Pasaka ambalo lina mafunzo mengi kwa jamii.
Punda wa Yesu alisema katika tamasha lake Msama anashirikisha waimbaji chipukizi, walemavu na wengineo ambao wanabeba dhana ya tamasha hilo ambalo dhamira yake ni kumuimbia na kumtukuza Mungu.
"Msama anajitambua waimbaji chipukizi na viongozi wa dini mbalimbali wanaohudhuria tamasha hilo, ivyo wengine nao waige mfano huo," alisema Punda wa Yesu.
Naye Honoratha Michael alitoa wito kwa Watanzania kujiandaa vilivyo na tamasha la Pasaka ambako pia alitoa wito kwa jamii kujitokeza kuwasaidia walemavu kama anavyofanya Msama.
Honoratha aliumia fursa hiyo kuwapa usia Watanzania wote wakiwemo walemavu kuiga mfano wa Msama ambaye anatekeleza majukumu hayo.

No comments:

Post a Comment