Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 16 February 2016

WAFANYAKAZI WA BANDARI WATINGA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA LEO

Baadhi ya wafanyakazi wa Bandari walioachishwa kazi mwaka 2008 wakiwa nje ya Wizara ya Katiba na Sheria leo hii.

Na Daniel Mbega
TAKRIBAN wafanyakazi 40 kati ya 992 waliopunguzwa kazi Bandari Januari 2008 leo hii wameandamana kutoka Mahakama Kuu ya Kazi, Kinondoni jijini Dar es Salaam hadi Wizara ya Katiba na Sheria wakilalamikia kucheleweshwa kwa kesi yao ya madai dhidi ya uongozi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).
Wakizungumza na FikraPevu nje ya makao makuu ya wizara hiyo, wafanyakazi hao wamesema kwa miaka nane sasa wamekuwa wakifuatilia madai yao ya kupinga kupunguzwa kazini pamoja na kupunjwa mafao, lakini licha ya madai yao kuonekana kuwa ya msingi, kesi hiyo imeendelea kucheleweshwa.
"Tumekuja hapa mahakamani leo baada ya kuambiwa kwamba kesi yetu ingetajwa, lakini tumeshangaa kusikia kwamba eti kesi hiyo ilitajwa jana Februari 15, 2016, imekuwaje sisi walalamikaji kupitia wakili wetu tupewe tarehe tofauti na mahaka nayo iwe na tarehe tofauti?" waliohiji wahanga hao na kuongeza kwamba kesi hiyo sasa imepangwa kutajwa tena Aprili 5, mwaka huu.
Aidha, walisema tukio kama hilo limepata kujitokeza Novemba 5, 2015 baada ya kuambiwa kesi yao imeahirishwa kutokana na sherehe za kuapishwa kwa Rais John Magufuli, lakini katika mshangao wao kesi hiyo ikatajwa Ijumaa Novemba 6, 2015 huku wao walalamikaji wakiwa hawana taarifa.
Wafanyakazi Bandari 1
Hali hiyo, wamesema, ndiyo iliyowalazimu kuandamana hadi Wizara ya Katiba na Sheria kupeleka kilio chao kutokana na kutumia gharama kubwa na kupoteza muda mwingi kufuatilia haki yao ambayo wamesema imekuwa mateso kwao.
Hata hivyo, wawakilishi wao ambao walikwenda kuonana na uongozi wa wizara, wametakiwa kuandika malalamiko yao na kuyawasilisha kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ili waone namna ya kulishughulikia suala hilo.
Wakili anayewawakilisha wafanyakazi hao kutoka kampuni ya Kalomo & Co. Advocates ya jijini Dar es Salaam hakuweza kupatikana kuzungumzia suala hilo kwa maelezo kwamba alikuwa mahakamani akisimamia kesi nyingine.
"Tunadai karibu Shs. 5 bilioni ambazo ni stahili zetu pamoja na usumbufu kwa miaka yote hii, kwa mujibu wa maelezo ya wakili wetu," alisema Nassoro Mohammed, mmoja wa wafanyakazi hao.
CREDIT: FIKRAPEVU

No comments:

Post a Comment