Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 10 February 2016

WACHEZAJI DR CONGO WATUZWA MASHANGINGI KWA KUTWAA UBINGWA WA AFRIKA WA CHAN

Wachezaji wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamezawadiwa magari ya kifahari baada ya kushinda Kombe la Taifa Bingwa Afrika kwa wachezaji wa ligi za nyumbani (CHAN).
Rais Joseph Kabila amemtunuku kila mchezaji gari gari la kifahari aina ya Toyota Prado la thamani ya $60,000 (£40,000).
Wachezaji hao pia wamepewa nishani, kwenye hafla iliyoandaliwa ikuluni.
"Asanteni sana kwa ushindi huu. Mmewaunganisha Wakongomani wote," alisema Rais Kabila.
Chui hao wa Kinshasa walitwaa kombe kwa kulaza Mali 3-0 kwenye fainali na kuwa taifa la kwanza kushinda kombe hilo mara mbili.
Mwaka 2009, mara ya kwanza kuandaliwa kwa michuano hiyo, DR Congo waliondoka na ubingwa kwa kulaza Black Stars ya Ghana 2-0 kwenye fainali.
Image copyrightAFP
Image captionDR Congo walilaza Mali 3-0 kwenye fainali
Mwandishi wa BBC Mbelechi Msochi anasema mchezaji Heritier Luvumbu Nzinga aliyeumia kwenye michuano hiyo pia ameahidiwa kwamba atasafirishwa ng'ambo kwa matibabu.
DR Congo
Image captionRais Kabila amewapongeza wachezaji wa timu ya taifa

No comments:

Post a Comment