Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 14 February 2016

TIMU YA MATOLA YAUA 8-0 NA KUPANDA LIGI KUU, TFF ‘YAFUTA’ MATOKEO

TIMU ya Geita Gold ya Geita jana ilishinda mabao 8-0 dhidi ya JKT Kanembwa katika mchezo wa mwisho wa Kundi C Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara, hivyo kujihakikishia kupanda Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Hiyo inafuatia waliokuwa wapinzani wao, Polisi Tabora kushindi mabao 7-0 dhidi ya JKT Oljoro katika mchezo mwingine wa mwisho wa kundi hilo jana.
Matokeo hayo yanazifanya timu zote zimalize na pointi 33 baada ya michezo yote 15, lakini Geita inayofundishwa na Suleiman Matola inaongoza kundi hilo kwa wastani mabao, ikiwa na wastani (GD) wa mabao 23 dhidi ya 22 ya Polisi.
Hata hivyo, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema halitatangaza timu iliyopanda Ligi Kuu kutoka Kundi C, hadi itakapoamuliwa na vyombo husika.
TFF imefikia hatua hiyo ili kupata nafasi ya kupitia taarifa za michezo kati ya JKT Kanembwa dhidi ya Geita Gold na Polisi Tabora dhidi ya JKT Oljoro iliyochezwa leo jioni katika mikoa ya Kigoma na Tabora.
“Taarifa za michezo hiyo kutoka kwa wasimamizi husika na vyanzo vingine vinakusanywa ili zifanyiwe kazi na vyombo husika vya TFF,”imesema taarifa ya TFF kwa BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE jioni ya leo.

CREDIT: BIN ZUBEIRY SPORTS

No comments:

Post a Comment