Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip
Mpango akiongea na wafanyabiashara nchini jijini Dar es salaam kuhusu Serikali inavyoshirikiana
na sekta binafsi katika kuinua uchumi wa
nchi ili kuweza kuwahudumia wananchi katika kupata huduma za jamii.
Nibu Waziri Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji (kulia) akiwa katika mkutano wa
wafanyabiashara nchini jijini Dar es salaam kuhusu Serikali inavyoshirikiana na
sekta binafsi katika kuinua uchumi wa
nchi ili kuweza kuwahudumia wananchi katika kupata huduma za jamii. Kushoto ni Kamishna
wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alfayo Kidata.
Makamu Mwenyekiti wa TPSF Salum Shamte
(kushoto) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa Waziri wa Fedha na
Mipango Dkt. Philip Mpango na wafanyabiashara nchini kuhusu Serikali
inavyoshirikiana na sekta binafsi katika kuinua uchumi wa nchi ili kuweza kuwahudumia wananchi
katika kupata huduma za jamii. Katikati ni Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.
Philip Mpango na kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt.
Servacius Likwelile.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dkt Reginald Mengi (kushoto) akiteta jambo na
Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Godfrey Simbeye (kulia) wakiwa katika mkutano wa
wafanyabiashara nchini jijini Dar es salaam kuhusu Serikali inavyoshirikiana na
sekta binafsi katika kuinua uchumi wa
nchi ili kuweza kuwahudumia wananchi katika kupata huduma za jamii.
Baadhi
ya wafanyabiashara wakiwa katika mkutano wa wafanyabiashara nchini jijini Dar
es salaam kuhusu Serikali inavyoshirikiana na sekta binafsi katika kuinua
uchumi wa nchi ili kuweza kuwahudumia
wananchi katika kupata huduma za jamii.
(Picha
na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
Na Eleuteri
Mangi-MAELEZO
Serikali imesema
dhamira yake ya kujenga uchumi wa viwanda nchini imejengwa kupitia maeneo ya
vipaumbele ambayo yataanza kutekelezwa katika bajeti ijayo ya mwaka wa fedha 2016/2017
kwa kutumia malighafi zipatikana nchini ikiwemo mzao ya misitu, kilimo, uvuvi
na madini ili kuwahudumia wananchi.
Hayo yamesemwa na
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango alipokuwa akiongea na wafanyabiashara
nchini jijini Dar es salaam.
Dkt. Mpango
aliyaeleza maeneo hayo ya vipaumbele ambayo yataanza kutekelezwa katika bajeti hiyo
ni pamoja na kuvirudisha viwanda vilivyobinafsishwa na kutafuta wabia ambao
wanaweza kufanyakazi iliyodhamiriwa.
Maeneo mengine ni
miradi mikubwa ya kielelezo ambalo wataalam wanalifanyiakazi ili kuweza kupata
matokeo makubwa, akitolea mfano Dkt. Mpango alisemas kuwa yapo maeneo maalum ya
kibiashara yakiwemo Bagamoyo, Kigoma na Mtwara kutokana na maliasili iliyopo
hapo.
Zaidi ya hayo, Dkt.
Mpango aliongeza kuwa ujenzi wa kiwanda cha chuma kwa kutumia malighafi
inayozalishwa kwa kutumia chuma kutoka Liganga na Mchuchuma itakuwa ni msingi
wa viwanda mama ikizingatiwa “Hakuna ujenzi usiohitaji chuma”.
Katika suala la
ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha Kimataifa, Dkt. Mpango alisema kuwa
mradi huo ni muhimu kwa lengo la kusukuma mbele sekta ya usafirishaji ndani na
nje ya nchi ikwemo nchi za Rwanda, Burundi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
(DRC) na mataifa mengine.
Mafanikio ya ujenzi
wa viwanda nchini yanawezekana kwa kwa kuwa Serikali imedhamiria kushirikiana
na serkta binafsi kwa kuwa maendeleo ya viwanda yanapaswa kuendana na maendeleo
ya watu kwa kuwapatia ajira, elimu inayoendana na mahitaji ya viwanda ili
maisha ya wananchi yawe bora zaidi.
Aidha, ili kujenga
uwezo wa kuwa na viwanda nchini, Serikali imejipanga kukusanya kodi ambayo
ndiyo msingi wa kuwa na uchumi imara utakaosaidia nchi kujiendesha ambapo
wafanyabiashara wote nchini wanapaswa kujisajili na kupewa namba ya usajili
(TIN) huduma ambayo inapatikana nchi nzima kupitia ofisi za Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA).
Katika mkutana huo,
Dkt. Mpango amewaasa wafanyabiashara kutunza kumbukumbu za biashara yao ili
kuwa na kumbukumbu ambazo zinatoa taarifa sahihi na kuhimiza wafanyabiashara
wenye mashine za kielekroniki (EFD) waendelee kuzitumia wanapouza bidhaa zao na
kuwaptia risiti wateja wao, kwa wale wasio na mashine hizo, Serikali inaendelea
kutekeleza agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Joseph Magufuli la kuwapatia mashine hizo.
Vile vile, Dkt.
Mpango ametoa namba za simu za
ofisi za TRA kitengo cha Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi ambapo wananchi
wanaweza kuwasiliana moja kwa moja na Idara ya Mambo ya Ndani TRA juu ya
maadili ya watumishi wa mamlaka hiyo nchi nzima kwa namba 0689122515 na kutuma
ujumbe mfupi kwa namba 0689122516.
Aidha, Dkt. Mpango
amewaonya wafanyabiashara ambao sio waaminifu waache kufanyabiashara za magendo
ambapo ameainisha baadhi ya maeneo yanayotumiwa ni pamoja na mwambao wa bahari
ya Hindi maeneo ya Mbweni, ziwa Victoria na ziwa Tanganyika.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa Kamati na Sera TPSF Felix Mosha
amesema kuwa Sekta binafsi itaendelea kushirikiana na Serikali katika
mpango wa kukuza uchumi wa nchi na kumhakikishia Waziri wa Fedha na Mipango kuwa watatimiza
wajibu wao wa kulipa kodi na kuhamasisha wafanyabiashara wote nchini wanakwenda
pamoja na Sera ya “Hapa Kazi Tu”.
No comments:
Post a Comment