Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 12 February 2016

KAMATI KUU YA ACT-WAZALENDO KUKUTANA JIJINI DAR ES SALAAM TAREHE 13 FEBRUARI 2016



Kamati Kuu ya Chama cha ACT-Wazalendo itafanya mkutano wa siku moja  kesho jumamosi  Februari 13/2016.

Mkutano utafanyika katika Ukumbi wa Kagame,Ulio katika hoteli ya Kagame nyuma ya kituo cha Mabasi Ubungo kuanzia saa 6:00 Mchana.

Kikao hicho ni cha  kwanza tokea kumalizika kwa Uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na Madiwani Oktoba 25 mwaka 2015

Mkutano huo wa Kamati Kuu utajadili  ajenda mbalimbali na baadhi ya ajaenda hizo  ni pamoja na hali ya kisiasa nchini ambayo itahusisha uamuzi wa Chama cha ACT-Wazalendo  juu ya kushiriki au kutokushiriki  katika uchaguzi wa visiwani Zanzibar kwa ajili ya kuwapata wajumbe wa Baraza la wakilishi pamoja na Rais wa Zanzibar.

Mbali na hilo pia kamati kuu itajadili ripoti ya matumizi ya fedha zilizotumiwa na Chama wakati wa Uchaguzi mkuu kwa ajili ya kuitoa taarifa hiyo hadharani, pamoja na mpango mkakati wa Chama wa muda mrefu 2016-2020 na ule wa muda mfupi wa 2016

Itakumbukwa kwamba mara ya mwisho, Kamati Kuu ya ACT Wazalendo ilifanya mkutano wake agosti mwaka jana kwa ajili ya kupendekeza majina ya wanachama watakaokiwakilisha Chama katika nafasi ya kugombea Urais na Umakamu wa Rais.

Abdallah Khamis
Afisa Habari ACT-Wazalendo
12/02/2016
0655-549154

No comments:

Post a Comment