Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday, 16 May 2015

WACHUNGAJI TAG TABORA WAONYWA KUHUSU UCHAGUZI MKUU


Na Hastin Liumba, NzegaKUELEKEA Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba mwaka huu, Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) mkoani Tabora limewatahadharisha  wachungaji na Viongozi wa Kanisa hilo kuchagua siasa ama kumtumikia Mungu lengo likiwa ni kuepusha udini katika mambo ya Kitaifa.

Hayo ya mesemwa na Askofu wa kanisa hilo Paul Meivukie katika Ibada ya uzinduzi wa sehemu ya Nzega Mashariki na kusimika viongozi watatu watakao simamia eneo hilo katika kutangaza neno la Mungu.
Meivukie akiwahutubia waumini wa kanisa hilo na wageni waalikwa alisema kuwa wachungaji wa kanisa  wanapaswa kuwa waangalifu katika kuelekea uchaguzi mkuu ilikudumisha amani iliyopo.
Alisema wachungaji wanapaswa kutotumika na kutumia makanisa kama mmoja ya majukwaa ya kisiasa wakati wa kampeni na kuongeza kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wachungaji watakaobainika.
Alisema kuwa endapo mchungaji akitaka kugombea nafasi mbalimbali katika uongozi anapaswa kuachia ngazi nafasi ya uchungaji wa kanisa,kukabidhi mara moja kitambulisho na nyaraka mbalimbali za kanisa.
Alisema kugombea nafasi za uongozi kwa jamii siyo dhambi badala yake kanisa ni mali ya jamii na kuongeza kuwa kanisa linawaombea wagombea wote na Taifa kwa ujumla lengo likiwa ni kudumisha amani.
‘’kugombea nafasi za uongozi siyo dhambi kwa wachungaji wetu lakini kanisa ni mali ya jamii hivyo hatuta kubali mchungaji awe kiongozi wa dini pia awe kiongozi wa serikali kanisa ni mali ya jamii hatufungamani  upande wowote wa siasa’’alisema Askofu Meivukie.
Akizungumzia upande wa waumini wa kanisa hilo Askofu alisema waumini hawana kipingamizi katika mapenzi yao dhidi ya vyama vyao hata hivyo aliweka angalizo la kutokutumia dini katika majukwaa ya kisiasa.
Mkuu wa wilaya ya Nzega Jackline Liana akiwa miongoni mwa viongozi waliohudhuria Ibaada hiyo alisema kuwa viongozi waliosimikwa wanapaswa kuwatumia wananchi na kulitumikia kanisa ilikuleta mabadiliko chanya.
Viongozi  walio simikwa ni pamoja na  Alex  Msambusi,Gabriel Mlawa na Endrwe  kayamba  ambao watakuwa sehem ya nzega mashariki katika kutangaza neno la mungu.
Endrwe  kayamba alisema kuwa uongozi huo unamalengo kadhaa yatayofanyika kwa kipindi kifupi ikiwa na kuongeza waumini wa kanisa hilo pamoja na kuongeza makanisa katika sehemu mbalimbali wilayani hapa.

No comments:

Post a Comment