Mkuu wa Kitengo cha Huduma za
Sheria kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Ester Riwa
(katikati) akiongea na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mbinga
Bw. Oscar Yapesa kuhusu ziara ya mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana wa Manispaa
ya Mbinga, wa kwanza kushoto ni Afisa Vijana kutoka Wizarani Bi. Amina Sanga.
Mkuu
wa Kitengo cha Huduma za Sheria Bi. Ester Riwa kutoka Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo aliyesimama akitoa mada ya ujasiriamali kwa Vijana wa
Halmashauri ya Manispaa ya Mbinga na jinsi ya kujikomboa kiuchumi.
Vijana
wa Halmashauri ya Manispaa ya Mbinga wameaswa kushirikiana na Serikali katika
kutafuta suluhisho la tatizo la ajira nchini ili waweze kujikomboa kiuchumi.
Rai
hiyo imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria Bi. Ester Riwa wakati wa
mafunzo elekezi kwa Vijana wa Halmashauri hiyo ya jinsi ya kujikwamua kiuchumi.
Bi.
Riwa alisema vijana wengi wamekuwa wakilalamikia ugumu wa maisha na kuacha
kujishughulisha na ujasiriamali hivyo kupelekea kukabiliana na ugumu wa maisha.
Katika
mafunzo hayo Bi Riwa alisema vijana wengi nchini wamekuwa wakitaka kupatiwa
pesa bila kuzingatia mafunzo ya elimu ya ujasiriamali hivyo kupelekea upotevu
na usumbufu katika urejeshaji wa marejesho.
“Nasikitishwa
na baadhi ya vikundi vya vijana katika Halmashauri mbalimbali wamekuwa
wakigomea mafunzo ya ujasiriamali na kudai posho za mafunzo na kusahau mafunzo
wanayapatiwa ni muhimu kuliko hiyo posho mnayoihitaji.
Katika
mafunzo hayo Bi. Riwa alisema Serikali haitoi posho za mafunzo ya ujasiriamali
bali hutoa elimu na baadae kutoa mikopo kwa vikundi vilivyosajiliwa kisheria.
Katika
hatua nyingine Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Bi. Amina Sanga alisema ili vijana waweze kupatiwa mikopo wanatakiwa
kujiunga katika vikundi na kuunda SACCOS ya Halmashauri ya vijana ambayo
itasimamiwa na vijana wenyewe.
Alisema
katika utoaji mikopo vigezo mbalimbali huzingatiwa ikiwa ni pamoja na umri wa
kuanzia miaka kumi na tano mpaka thelathini na tano.
Akizungumzia
kigezo cha umri Bi. Sanga alisema kigezo hicho ni kwa mujibu wa Sera ya
maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007 ambapo sera hiyo inamtambua kijana ni kuanzia
umri wa miaka 15 mpaka 35.
Kuhusu
suala la urejeshaji wa mikopo yote Bi Sanga alisema ni wa kipindi kisichozidi
miaka miwili na muda wa maandalizi miezi mitatu ambapo kikundi kitalazimika
kulipa tozo ya asilimia 15 iwapo kitashindwa kurejesha mkopo katika muda
uliopangwa.
Hivyo
amewataka vijana kuandika maandiko ya kupatiwa mikopo kwa ushirikiano na Afisa
Vijana wa Halmashauri yao na maandiko yao yatawasilishwa Wizarani na
kuchambuliwa kwa ajili ya kupatiwa mikopo kwa vikundi vitakavyokidhi vigezo
ambapo kikomo cha mkopo kwa kikundi ni kiasi kisichozidi shilingi miloni kumi
kulingana na uhalisia wa mradi wa kikundi husika.
No comments:
Post a Comment