Mradi wa Kilimo cha Tangawizi wa kikundi cha ujasiriamali cha Ushindi kilichopo katika kijiji cha Mkongotema kata ya Mkongotema tarafa ya Madaba Halmashauri ya Songea.
Na Benjamin Sawe
Katika
ulimwengu wa sasa wenye changamoto kubwa ya ukosefu wa ajira na ushindani wa
kila namna ujasiriamali unabaki kuwa dhana pekee inayoweza kuwakomboa vijana
kiuchumi na kuwawezesha kutimiza malengo na ndoto walizonazo.
Kutokana
na kukithiri kwa idadi kubwa ya vijana wanaohitimu katika ngazi mbali mbali za
elimu hasa elimu ya msingi,sekondari na
Chuo ile hali hawana ajira na kuishia
kukaa mitaani kutokana na elimu waliyoipata iliwaandaa kuajiriwa maofisini na
sio kujiajiri,ni ukweli usiopingika kwamba elimu ya ujasiriamali inahitajika
kwa kiasi kikubwa ili kuleta ukombozi wa kweli wa kiuchumi.
Mafanikio
ni shilingi yenye pande mbili kuajiriwa na kujiajiri ,vijana wasifikiri kuwa
kuajiriwa ndio njia pekee ya kufanikiwa
pia wajue kuwa kuna mafanikio ya
kiuchumi nje ya ajira na haya ni kwa wale walioamua kujiajiri kwa kuanzisha
miradi mbali mbali ama biashara na huo ndio ujasiriamali wenyewe.
Vijana
wengi wamekuwa wakihuzunika, kunung’unika na kulalamika kana kwamba waliambiwa
maisha ni rahisi. Wakati unapoukubali ukweli ya kuwa maisha ni magumu, ndiyo
wakati ambao maisha hayawi magumu tena! Ndiyo! Kwa sababu ukijua maisha ni magumu
lazima utaishi kwa nidhamu kubwa, na nidhamu ndiyo msingi namba moja wa kutatua
matatizo yote katika maisha.
Ukiona
unalalamika kuwa maisha ni magumu, rejea katika fikra zako, huenda bado
hakujafanyika mapinduzi! Ukiona unaukubali ukweli kuwa maisha ni magumu na
wakati huo huo huna nidhamu, ama una nidhamu chache, basi ujue kuwa hujaukubali
ukweli wote kuwa maisha ni magumu!
Ujasiriamali
kwa ujumla ni dhana ambayo ili kukubalika kikamilifu, kunahitajika mapinduzi
makubwa ya fikra kwa vijana kuliko elimu ya kawaida. Fikra za kuwatazama
wajasiriamali waliofanikiwa na kutoa visingizio kuhusu mafanikio yao, ni fikra
zenye matege na ukilemaa na hizo kamwe haziwezi kutufanya tukafanikisha
kujikwamua kiuchumi.
Kutokana
na hali hii, utagundua kuwa tatizo linalowakabili vijana wengi wa Tanzania
katika kujikwamua kiuchumi si mitaji wala ukosefu wa elimu, bali ni la kifikra.
Ili kijana aweze kufanikiwa kubuni na kuanzisha mradi, anatakiwa aamini kuwa
kujiajiri kuna tija kubwa sawa na kuajiriwa. Kwa sababu ni mara chache mtu
anaweza kuwa tajiri kwa kutegemea mshahara wake pekee!
Ni
vema vijana wote wafahamu kuwa “fedha ni mawazo.” Kama fedha ni mawazo basi
kujikwamua kiuchumi ni mawazo pia. Kama ni suala la kuwaza, kwa nini asiye na
elimu asiwaze? Kama ujasiriamali unaanza na mawazo, kwa nini wenye elimu
walilie mitaji? Sikatai kuwa mitaji ni suala la msingi katika ujasiriamali,
lakini ifahamike kuwa uthubutu wa kuanza na kujaribu wazo hata kwa sehemu ndogo
ndiyo msingi wa mafanikio ya mjasiriamali yeyote.
Nchi
ya Tanzania ina ajira na fursa nyingi za kiuchumi za kumtosha hata mtoto
atakayezaliwa kesho! Sioni sababu ya mhitimu wa darasa la saba kukosa ajira,
kwanini mhitimu wa kidato cha nne na sita wakose kitu cha kufanya chenye
kuwakwamua kiuchumi katika nchi tajiri kama Tanzania? Kwa wale ambao ni
wahitimu wa vyuo vya kati na vya elimu ya juu, sioni haja ya kuwaandikia kwa
sababu inatosha sana kwao kutengeneza ajira kwa wengine.
Tatizo
jingine linalowasibu vijana wengi wa Tanzania kiasi cha kushindwa kupoka
(seizing) fursa za kijasiriamali na fikra potofu za kutaka kuanza na mafanikio.
Kama ni kijana msomi anawaza kuanza na kampuni yenye mtaji wa mamilioni.
Yatatoka wapi mamilioni bila kuanza na kidogo? Kwa wale ambao hawana elimu
kubwa wengi wamevia kimawazo kwa kuota kuokota fedha ama kuokota elimu!
Kama
ulikosa elimu hupaswi kulalamika wala kunung’unika kwa sababu huko ni kupoteza
muda, bado unayo nafasi kubwa ya kufanikiwa. Fikra za kupata vya bure bila
kuhangaika ndiyo zinazosababisha Watanzania wengi kujiingiza katika michezo
mingi ya bahati nasibu kwa matarajio kuwa watatoka! Cha ajabu ni kuwa michezo
hiyo, ama mingineyo inawapotezea fedha badala ya kuwasaidia, hapa yanahitajika
mapinduzi ya kifikra.
Maisha
bora na ya uhakika kwa vijana yanawezekana ikiwa kutafanyika mageuzi makubwa
katika sekta binafsi, ujasiriamali. Ili ujasiriamali ufanikiwe na kufanywa na
vijana kwa uhakika, lazima vijana wote wakubali kufanya mapinduzi ya fikra zao
za kitegemezi.
Tukisema
ujasiriamali hatumaanishi ujasiriamali wa kujikwamua wewe kijana peke yako,
bali tunagusa pia katika utanuzi wa fikra za kuanzisha kampuni, huduma na
bidhaa mbalimbali zenye ubunifu mpya kwa kuvitumia vipaji kikamilifu.
Vijana
wengi wamekuwa wakilalamikia ugumu wa maisha na kuacha kujishughulisha na
ujasiriamali hivyo kupelekea kukabiliana na ugumu wa maisha.
Mkuu
wa Kitengo cha Huduma za Sheria Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi.
Ester Riwa akitoa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana wa mkoa wa Ruvuma anasema
vijana wengi nchini wamekuwa wakitaka kupatiwa pesa bila kuzingatia mafunzo ya
elimu ya ujasiriamali hivyo kupelekea upotevu na usumbufu katika urejeshaji wa
marejesho.
Anasema
baadhi ya vikundi vya vijana katika Halmashauri mbalimbali wamekuwa wakigomea
mafunzo ya ujasiriamali na kudai posho za mafunzo na kusahau mafunzo
wanayapatiwa ni muhimu kuliko hiyo poshowanayodai.
Bi
Riwa anasema Serikali haitoi posho za mafunzo ya ujasiriamali bali hutoa elimu
na baadae kutoa mikopo kwa vikundi vilivyosajiliwa kisheria.
Kaimu
Mkuu wa Mkoa Mh.Norman King anasema Serikali imeamua kutoa mafunzo kwa vikundi
vya vijana ya jinsi ya kuandaa maandiko ya miradi mbalimbali, uongozi bora na
stadi za maisha ili kuwatoa katika mitazamo hasi kwenda mitazamo chanya kwa
kutumia fursa zilizopo.
Anasema
vijana wengi wanafursa mbalimbali za kujikwamua na umaskini lakini hawatumii
fursa hizo vizuri na kubakia wakikaa vijiweni bila kujishughulisha na kazi
yeyote na kuishia kuvuta madawa ya kulevya na kuwa wezi.
Nea
Diwani wa kata ya Matimila jimbo la Peramiho Mh. Menesi Komba amesema mafunzo
ya kujengewa uwezo ni fursa kwa vijana wa Halmashauri ya Songea kwani watakuwa
wamepewa uelewa mkubwa wa jinsi ya kuendesha shughuli zao za ujasiriamali kwa
ufanisi na utaalamu
Anawaasa
vijana kutekeleza elimu ya ujasiriamalikwa vitendo kwa kuwafundisha vijana
wenzao ambao hawakupata bahati ya kuhudhuria katika mafunzo hayo na kuachana na
tabia ya kuwa wabinafsi wa kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vikundi vingine.
Tubadili
mitazamo ya kuwaona ni sehemu ya matatizo katika jamii bali tuwaone kama ni
sehemu ya suluhisho la matatizo yaliyopo kwenye jamii kwasababu vijana wana
nguvu,vipaji,uwezo wa ajabu,ubunifu .
Nguvu
za vijana zikitumika vizuri zinaweza kufukuzisha umasikini,utegemezi na
matatizo lukuki yanayoikumba jamii.
Vijana
nao wasikae nyuma katika masuala ya kifamilia ,kijamii,wawajibike watumie nguvu
walizonazo,ubunifu,uwezo,vipaji na talanta na elimu walizonazo katika kutatua
changamoto za jamii badala ya kukaa kama watu wa pembezoni.
Ni
vyema kuhamasisha ushiriki mpana wa vijana katika masuala ya kiuchumi,kijamii
na kisiasa kwasababu vijana wakiachwa nyuma hali itazidi kuwa mbaya kwa vizazi
vijavyo.
“Nusu
ya maisha tunayoishi yanatokana na kizazi kilichopita na nusu nyingine
inatokana na kizazi kilichopo” Anaeleza Mtunzi mmoja wa kitabu
Ina
maana kuwa vijana wanawajibika kuweka misingi bora ya kiuchumi,kimaadili na kiuwajibika misingi ambayo itatumiwa na
kizazi kijacho iwapo hawatafanya hivyo hali itazidi kuwa mbaya .
“Unapoacha
kutimiza wajibu wako duniani,kutumia uwezo ulionao,vipaji unapokufa unaacha nafasi wazi duniani ambayo
ingepaswa uijaze kwa kuacha kitu duniani kizazi kijacho kikija kitakuta nafasi
uliyoiacha hukufanya kitu” Anaeleza Mtunzi Mashuri wa vitabu Myles Munroe.
No comments:
Post a Comment