
Tahadhari ya Tsunami inayosambazwa kwenye mitandao ya Jamii sio ya
kweli.
Kumekuwapo na taarifa zinazosambazwa kwa njia ya mtandao wa simu
kuhusiana na uwepo wa tsunami kati ya kuanzia saa 1 usiku na saa 3 usiku leo
hii siku ya Ijumaa tarehe 8/5/2015.Taarifa hiyo imemtaja Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Hali ya Hewa na Televisheni ya Taifa (TBC) kutoa tangazo hilo.
Taarifa hizo si za kweli unaombwa umjulishe na mwenzio.
Aidha, Mamlaka inapenda kutoa wito kwa umma kuacha kutoa taarifa za
kupotosha katika mitandao ya kijamii.
Imetolewa na:
Kitengo cha Uhusiano
No comments:
Post a Comment