Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 26 May 2015

POLISI WAPAMBANA NA AL SHABAAB KENYA

Wanamgambo wa Al Shabaab
Askari mmoja ameripotiwa kujeruhiwa baada ya kuwepo kwa mapambano makali kati ya Polisi na Wanamgambo wa Al Shabaab Kaskazini Mashariki mwa Kenya.

Wizara ya usalama wa Taifa nchini Kenya imethibitisha kuwa askari mmoja amejeruhiwa wakati wa shambulizi la Wanamgambo wa alshabaab katika kijiji cha Yumbis mjini Garissa, Kaskazini Mashariki mwa Kenya.
Msemaji wa wizara hiyo Mwenda Njoka ameiambia BBC kuwa kulikuwa na makabiliano makali kati ya Polisi na wapiganaji hao.
Viongozi katika eneo hilo wamesema Magari manne ya Polisi yamechomwa moto na wanamgambo. Polisi wameiambia BBC kuwa wamepeleka kikosi kuimarisha hali ya usalama.
Taarifa za awali zilieleza kuwa askari kadhaa wanahofiwa kufa kwenye kwenye shambulio la usiku wa jumatatu.
Wakati huo huo al shabaab wamedai kuhusika katika shambulio hilo wakidai kuwa wamewaua Polisi 20, lakini vyombo vya usalama vimesema madai hayo ni Propaganda.
Siku ya jumatatu Polisi watatu walijeruhiwa baada ya Gari lao kukanyaga Bomu la kutegwa ardhini.
Kikosi cha askari 20 kilifika katika eneo hilo kuwasaidia waliojeruhiwa wanaoelezwa kushambuliwa na Al Shabaab.
Al shabaab wamekiri kuhusika katika shambulio hilo na kuchoma magari mjini Garissa.Msemaji wa kundi hilo Shaykh Abdiasis Abu Mus’ab amesema shambulio hilo limefanywa na kikosi maalum kiitwacho ‘mujahidin’.
Mus’ab amesema shambulio lilikuwa la “mafanikio” na kudai kuwa hasara waliyoipata askari wa Kenya ni kubwa.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment