Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 6 May 2015

POLISI TABORA LAWAMANI KWA KUBAMBIKA KESI

IGP Ernest Mangu
Na Mwandishi Wetu, Tabora
JESHI la polisi mkoani Tabora limelalamikiwa na kutuhumiwa kwa kumbambika kesi Bilali Saidi Masangura ya wizi wa TV na sh milioni 200.



Akiongea muda mfupi kituo kikuu cha polisi mkoani Tabora kabla ya kupelekwa wilayani Urambo anakotuhumiwa wizi wa TV alisema hana hatia juu ya kesi hizo mbili.

Bilali Masangula alisema alikamatwa mkoani Morogoro akiwa njiani kuelekea Dar-es-Salaam katika biashara zake za mahindi.

‘Nilikuwa safarini toka Mwanza kuelekea jijini Dar-es-Salaam katika biashara zangu nilikamtwa nikaletwa mkoani Tabora na kufunguliwa kesi hizo," alisema.

Alisema baada ya kukamatwa alirejeshwa mkoani Tabora na kufunguliwa mashitaka ya wizi wa sh milioni 200 za kampuni moja (jina linahifadhiwa).

Aidha alibainisha kuwa kesi hiyo ilifanyiwa uchunguzi wa kina na mwisho wa siku ilionekana sina hatia na kesi kufutwa.

Alisema baada ya kufutwa kwa kesi hiyo ghafla tena alikamatwa na kufunguliwa kesi nyingine ya wizi wa TV wilayani Urambo.

Aidha alisema kesi hiyo amefunguliwa baada ya kusota rumande kwa siku 23 bila ya kupelekwa mahakani huku akinyimwa dhamana na kupewa vitisho.

Alisema yeye biashara zake ni Mahindi na ana duka la simu za kiganjani anauza "sasa huo wizi ninaotuhumiwa ni njama za baadhi ya polisi kunibambika kesi."

Alisema anasikitishwa na polisi hao kwani dhamana alinyimwa huku akisota rumande siku 23 bila kupelekwa mahakamani kama sheria zinavyosema.

Alisema ameamua kuongea na waaandishi wa habari ili umma ujue uonevu anaotendewa na polisi akiwa hana kosa lolote.

Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora Kamishna msaidizi (ACP) Suzan Kaganda alipoulizwa malalamiko hayo alisema hana taarifa za Bilali Masangura kubambikwa kesi.

Kamanda Kaganda alisema licha ya kutokuwa na taarifa hizo atafuatilia lakini akasema hakuna ndugu wala huyo Bilali aliyewasilisha malalamiko kwake.

‘Sijaona mtu yoyote wala hao wanaolalamika kubambikwa kesi ili niweze kuchukua hatua zaidi……waje tu kuniona niweze kujua nini kinaendelea,” aliongeza.

No comments:

Post a Comment