Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 6 May 2015

CHAWATIATA TABORA YAWALILIA ALBINO


Na  Hastin Liumba, Tabora
WAGANGA wa kienyeji wametakiwa kutojihusiha na vitendo vya  mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi(Albino ) pamoja na vikongwe  ikiwa ni pamoja na kulipia nyara za Serikali wanazozitumia katika kutekeleza kazi zao.


Kauli  hiyo imetolewa na mwenyekiti wa Chama Cha Waganga na tiba asilia (CHAWATIATA) Manispaa ya Tabora  Ramadhani Rajabu alipokuwa akizungumza na  Mtanzania Nyumbani kwake kuhusu tuhuma zinazo wakabili kujihusisha na mauji hayo.
Alisema ataungana na kauli ya Serikali ya kuwakamata waganga wanaojihusisha na vitendo hivyo ikiwa ni pamoja na wale wanao tumia ramli chonganishi kwani wanaweza kuondoa amani ya nchi yetu ikiwa ni pamoja na kuwapa hofu  ya kuishi albinism.
Alisema kila wilaya inatakiwa kuwatambua waganga wa kienyeji wanaopatikana na wenye  vibali vya kutibu kutoka kwenye chama na endapo atabainika kwenda kinyume na mashariti ya katiba ya chama atachukuliwa hatua kari za kisheria na kufikishwa mahakani ili kujibu tuhuma itakayo kuwa inamkabili.
“Haiwezekani mganga ambaye anatibu ama kutoa tiba ya kweli amshawishi mteja wake kuleta viuongo vya maalbino huyo siyo mganga na hakuna tiba yoyote ya asili inayo tumia kiungo cha binadamu isipokuwa viungo vya wanyama wengine hapo inawezekana.”alisema Rajabu.
Alisema inasikitisha  sana  kuona waganga wa tiba asili wanatuhumiwa kuhusika na mauaji ya albino  pamoja vikongwe jambo linalotia wasiwasi hasa kwa waganga wengine ambao wanatiba nzuri huku wakiharibiwa na baadhi watu ambao ni matapeli yaani watu wenye tamaa ya fedha hali ambayo haiwezi kuvumilika,lazma hatua zichukuliwe dhidi yao.
Jamii itambue hakuna Mganga ambaye anaweza kumwagiza mteja wake kumletea kiungo cha albno ili kuweza kutibiwa kwani hata waganga wana watoto ambao ni albinism.
Aidha alisema  Serikali inatakiwa kulitambua hili kama janga la kitafaifa na siyo kwamba mauaji haya yanawahusu wanganga wa kienyeji kama inavyononekana bali inatakiwa kuakaaa chini na kulitafitia
Hata hivyo aliowamba wanachi kuungana kwa mpamoja kuhakikisha ulinzi dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi unapatikana na kutoa taairfa sehemu inayohusika pale inapotokea albino au kikongwe kufanyiwa unyama.
Rajabu ameyataka medhehebu yote ya dini kuungana kwa pamoja kuliombea taifa juu ya janga hili la mauaji ya albino na vingongwe linalozidi kushika kasi kote nchini ikiwa ni pamoja kulipa taifa sifa mbaya kwenye mataifa ya nje.

No comments:

Post a Comment