Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 24 May 2015

CHAMA CHA WAENDESHA BODABODA TABORA KATIKA MGOGORO MKUBWA WA FEDHA

Waendesha boda boda Tabora wakionyesha mshikamano katika mazishi ya dereva mwenzao Novemba 2014. Chama hicho sasa kimeingia katika mgogoro. (Picha kwa hisani ya Alyson.com).

Na Mwandishi Wetu, Tabora
UONGOZI Chama cha waendesha Bodaboda mkoani Tabora (TTMA) kimeingia kwenye mgogoro wa kimaslahi na baadhi wanachama ukituhumiwa kutafuna kiasi cha Shs. 1.6 milioni na kuuza pikipiki za chama na kugawana fedha.


Wakiongea kwa nyakato tofauti wanachama hao ambao hawakuwa tayari kutajwa majina walisema kiasi hiho cha fedha kimetafunwa baada ya kuuzwa kwa pikipiki moja iliyotolewa na mjumbe wa mkutano mkuu taifa Emmanuel Mwakasaka.

Wanasema viongozi waliotafuna kiasi hicho baada ya kuuzwa kwa pikipiki hiyo waligawana Shs. 400,000 kila mmoja.

Walitaja viongozi hao kuwa ni Waziri Kipusi (mwenyekiti), Shaban Juma Maregesi (makamu mwenyekiti),Ali Hailala (Katibu mkuu) na Kassim Kiduli (katibu mwenezi).

Aidha tuhuma nyingine ni viongozi hao kuidanganya kamati kuu tendaji kuweka mwanasheria kutumika kuandaa katiba ya hama chao kwa gharama ya Shs. 170,000 na zikatumika zaidi ya Shs. 520,000.

Aidha walisema mkuu wa mkoa wa Tabora wakati huo Fatma Mwassa alitoa pikipiki mbili mwezi septemba 28,2013 kwa chama hicho ili zikopeshwe kwa wanachama lakini uongozi haukufanya hivyo hadi leo hii.

Mwassa alitoa pikipiki hizo siku ya uzinduzi wa ofisi za chama hicho mradi ambao ulijulikana kama ‘Fatma Mwassa Foundation’ lakini kinyume na hapo hadi leo wamekwenda kinyume na makubaliano na mkuu wa mkoa.

Aidha tuhuma nyingine za viongozi hao ni kuidanganya kamati kuu tendaji kuhusiana na mradi wa Autozone Ltd wa kutengeza vibao vya magari na pikipiki katika ya Oktoba Mosi, 2014 na Oktoba 30,2014.

Aidha uongozi huo ulikula njama na kudai kuna mtu anatakiwa kulipwa Shs. 2 milioni kama posho ambaye yuko serikalini mkoa wa Tabora ili mradi huo uanze na kuwaletea wateja wengi.

Aidha waliongeza mwezi Oktoba 2014 na mwezi Novemba 2014 utekelezaji wa malipo hayo yasiyo rasmi yalianza na kiasi cha Shs. 350,000 kililipwa.

Wanasema walipotafuta ukweli waligundua malipo hayo yalifanyika na fedha hizo hazikenda kokote wala hakuna mtu toka serikali aliyelipwa kiasi cha Shs. 350,000 za awali kati ya Shs. 2 milioni.

Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Bodaboda mkoani Tabora (TTMA) Waziri Kipusi alipoulizwa kwa niaba ya viongozi wenzake alikana tuhuma hizo na kudai za kuupaka matope uongozi wake.

“Siyo kwenye katika hilo mimi nachafuliwa na wasiokitakia mema chama chetu fedha hizo zinazodaiwa nimekula na wenzangu hata kesho wafanye ukaguzi zinajidhihirisha ukweli wake.” alisema.

Alipotafuwa kwa mara nyingine aligoma kutoa maelezo zaidi.

No comments:

Post a Comment