Ney wa Mitego akishambulia jukwaa Singida
Stamina na Ney wa Mitego wakiimba pamoja
Baraka da Prince naye hakuwa nyuma
Mr Blue
Kutokana
na umati mkubwa uliojitokeza mwaka jana mjini Singida, wadhamini wakuu wa
tamasha hilo, kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake maarufu cha
Serengeti Premium Lager waliamua kuwarudisha nyuma mashabiki wa mkoa huo kwa
kuwapa shoo kali.
Kwa mara nyingine tena Singida
walifanikiwa kuweka historia katika
mfululizo wa matamasha hayo miaka ya hivi karibuni kwa kujitokeza kwa idadi
kubwa, tiketi zilinunuliwa tangu saa 10 alasiri toka kwa wauzaji na mashabiki
waliokuwa na shauku kubwa ya kushuhudia burudani.
Wasanii waliojitokeza kuisindikiza
SBL katika shoo hiyo ni pamoja na “Mwana Fa, Nikki II, Makomando, Stamina, Ney,
Young Killa, Linah, Recho, Mr. Blue, Dully Sykes, Mo Music, Baraka Da Prince,
Supa Nyotas:- (G-Luck, K-Style and Edo boy) ambao walitoa burudani safi
iliyoacha gumzo kwa mashabiki wa Singida na vitongoji vyake.
Makomando, Ney na Stamina ni baadhi
ya wasanii waliowashika mashabiki wa mkoa huo kwa shoo kali wakati walipopanda
katika jukwaa na kutumbuiza na nyimbo kama “Kibababa” na “Huko kwenu vipi”
ambazo ziliwakamata vilivyo mashabiki wa burudani uwanjani hapo. Dully Sykes ni
msanii mwingine aliyewakamata mashabiki kwa kutoa burudani nzuri mara baada ya
kupanda jukwaani na kuwafanya waimbe pamoja nae na kumshangilia alipokuwa akiimba.
“Tamasha la Serengeti Fiesta hapa
Singida limegeuka kuwa la kushangaza kwetu kama waandaaji na kiukweli hii ni
moja ya shoo kali na ya kusisimua ambayo hatukutarajia kama ingewafurahisha
mashabiki wetu wa Singida kiasi hiki,”....alithibitisha Ndugu Rugambo Rodney,
Meneja Chapa Serengeti Premium Lager.
Serengeti
Fiesta inatarajia kuhitimisha ziara zake za mwaka huu hapo tarehe Oktoba 18
jijini Dar es Salaam, mikoa mingine inayotarajia kupata shoo murua za Serengeti
Fiesta ni pamoja Dodoma na Mtwara kama walivyo ahidi waandaji.




No comments:
Post a Comment