Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 27 October 2014

WABUNGE WAMBANA MKURUGENZI AONYESHE ZILIKO SHS. 100 MILIONI

Naomi Nnko, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (Laac), imemshukia mkurugenzi wa halmashauri ya Magu na kumtaka atoe maelezo kuhusiana na zilipo zaidi ya Sh.100,000,000.80 za miradi ya  maendeleo zilizotolewa na serikali mwaka 2012/2014. 


Kamati hiyo imemtaka mkurugenzi huyo kutoa maelezo hayo kabla ya kamati hiyo haijaondoka mkoani Mwanza wiki hii.

Akizungumza katika kikao cha ukaguzi wa hesabu za halmashauri hiyo, Mwenyekiti wa Laac, Rajab Mbaruku, aliyefuatana na wajumbe tisa wa kamati hiyo, alimtaka mkurungenzi huyo, Naomi Nnko, kutoa maelezo ya kina juu ya fedha hizo ambazo hazifahamiki zilipo na nyingine zikiwa zimetumika kinyume.

“Tunahitaji kupata maelezo juu ya fedha za wanawake, vijana, walimu waliofariki ili tufahamu zilipo,” alisema Mbaruku.

Akijibu tuhuma hizo mkurugenzi huyo alidai kuanzia Oktoba 2012 alianza kazi na kukuta baadhi ya madeni yaliyoachwa na aliyekuwa mkurugenzi, Koronel Ngudungi, ambaye alihamishwa Ngara baada ya kufanya vibaya.

“Madeni haya ya fedha ni ya kipindi cha nyuma, Ngudungi aliacha madeni mengi katika halmashauri hii, fedha nilizotumia nilizihamisha kutoka katika akaunti nyingine na kuzipeleka katika matumizi ya maendeleo ya wilaya hii,” alisema Nnko.

Hata hivyo, kamati hiyo haikuridhishwa na maelezo hayo na kumtaka mkurugenzi kupeleka maelezo ya kina kabla ya siku ya majumuisho licha ya juhudi za maendeleo ya wilaya hiyo zikionekana ikiwamo ujenzi wa jengo la makao makuu ya halmashauri ya wilaya Magu, itakayogharimu Sh. bilioni sita.

Miradi mingine ya halmashauri hiyo ambayo ipo chini ya mkandarasi wa halmashauri hiyo, Mhandisi Simon Nkuru, imeshindwa kuendelea kutokana na ukosefu wa fedha kwa awamu ya pili hasa ujenzi wa jengo la halmashauri huku ujenzi wa mabweni mawili ya shule ya sekondari Magu, zahanati wadi ya wanaume kata ya Rugeye, nyumba za watumishi na madarasa ya Shule ya Sekondari Rubugu yakikamilika.

Mjumbe wa kamati hiyo, Ezekiel Maige, alisema idara ya uhasibu na ukaguzi wa ndani katika halmashauri hiyo umekuwa ni mzigo kwa serikali na kuonyesha dhahiri kushindwa kutekeleza majukumu yake.

Naye Azah Mohamed, aliwapa tahadhari makandarasi wa halmashauri atakayeshindwa kutimiza wajibu wake, atawajibishwa kisheria.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment