Amiri jeshi mkuu wa jeshi la Burkina Faso Jenerali Honore Traore ametangazwa kuvunjwa kwa serikali na bunge la taifa.
<span >Jenerali Traore hata hivyo hakutangaza ni nani atakayechukua uongozi wa taifa hilo.
Jenerali Traore aliwaambia waandishi wa habari kuwa kutaundwa serikali ya mpwito baada ya kufanyika mazungumzo baina ya wanasiasa wa upinzani na kiongozi Bwana Campaore.
Jenerali Traore alikuwa akiwahutubia waandishi wa habari baada ya kushuhudia fuzo la maandamano katika mji mkuu wa <span >Ouagadougou.
<span >Waandamanaji walivamia majengo ya bunge na majumba ya wafuasi wa rais<span >Blaise Compaore wakipinga azimio lake la kutaka kubadilisha katiba ya taifa ilikumruhusu kuwania kipindi kingine cha uongozi baada ya kutawala kwa zaidi ya miaka 27.
Awali <span >Waandamanaji waliteketeza majengo ya Bunge mjini Ougadougou, na kuwafurusha wabunge .
Runinga ya itaifa ililazimika kusitisha matangazo baada ya waandamanaji kuvamia shirika la utangazaji.
Waandamanaji kisha wameelekea Ikulu ya Rais na wanajeshi wamekua wakiwafyatulia risasi.
Vilevile baraza la jiji pamoja na makao makuu ya chama tawala yameteketezwa moto.
Umati mkubwa wa watu umeonekana ukielekea ikulu ya Rais huku uwanja wa ndege ukifungwa.
Rais Blaise Compaore ameomba utulivu ,katika ujume aliotumwa kwa Twitter.
Wabunge wamelazimika kuahirisha kura hiyo ya kubadilisha katiba kumkubalia Compaore kuwania tena Urais mwaka ujao.
Watu watano wameuawa katika maandamanao hayo ambayo yametajwa kuwa mabaya zaidi kukumba utawala wa Blaise Compaore.
Awali wanajeshi waliwafyatulia risasi waandamanaji waliovamia majengo ya bunge.
Compaore alitwaa madaraka kupitia mapinduzi mwaka wa 1987.
Amekua akishinda uchaguzi lakini kura hio hukumbwa na utata.
Ufaransa na muungano wa Ulaya zimemuomba Rais Compaore kutobadilisha katiba ili kuwania tena.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment