Mwanafunzi wa chuo kikuu nchini Misri ambaye hufanya kazi ya kupiga picha na uandishi wa runinga wa kituo cha Al- Jazeera amekamatwa na kuwekwa korokoroni.
Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 21,ambaye jina lake halikufahamika mara moja ,alikamatwa na askari kanzu wakati akipiga picha wakati wa maandamano katika mji wa Mahalla,ulioko upande wa kaskazini mwa mji mkuu Cairo.
Mwandishi na mpiga picha huyo alikuwa na kijitabu kidogo chenye maandishi na maneno yanayotumiwa jeshini na polisi.waandishi wawili waliokuwa pamoja naye wakiwa na kamera walifanikiwa kukimbia.
Mwezi June mwaka huu nchi hiyo iliwafunga waandishi wawili wa Al-Jazeera miaka saba gerezani na mwingine watatu, alihukumiwa miaka kumi gerezani kwa kosa la kusambaza habari za uongo na kuunga mkono kundi lililopigwa marufuku la Muslim Brotherhood.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment