Mahakama nchini Saudi Arabia imetoa hukumu ya kifungo cha miaka mitano mpaka nane kwa wanasheria watatu nchini humo, kwa kosa la kukosa mfumo wa haki za nchi katika mtandao wa kijamii blogs na twitter.
Shirika la habari nchini Saudi Arabia limesema kuwa wanasheria hao wamepatikana na hatia ya kuwadharau watawala na kudharau mfumo wa mahakama wa nchi hiyo.
Mahakama imesema wanasheria hao watazuiliwa kufanya mawasiliano na jamii pamoja na chombo chochotete cha habari nchini humo.
Hata hivyo mahakama imeonya watumiaji wa mitandao ya kijamii kwamba watafuatiliwa na kupata adhabu sawa na wanasheria hao.
Nchi ya Saudi Arabia imeonyesha uvumilivu kidogo kwa raia wanaopinga serikali tangu ilipoanza mwaka 2011.
CREDIT: BBC/SWAHILI
No comments:
Post a Comment