Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema na Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa
MAKUBALIANO SABA YA UKAWA.
1. SERA,-Kudumisha sera za vyama vyote vinne na kuchukua mambo yanayofanana ili kuvifanya viwe na kauli ya Pamoja.
2.WAGOMBEA,-Kusimamisha
wagombea wa pamoja katika chaguzi zote za Serikali za Mitaa, Wabunge, Baraza la Wawakilishi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Rais wa Zanzibar.
3.UTARATIBU,-Namna
gani vyama vitashirikiana katika uchaguzi wa serikali za Mitaa na
uchaguzi Mkuu na kusambaza Mwongozo katika mikoa mbalimbali kuwaelekeza
viongozi mambo yanayotakiwa.
4.KURA YA HAPANA,-Kushirikiana
katika mchakato wa kupiga kura ya hapana katika kura ya maoni ya katiba
inayopendekezwa kwa kuwa haijazingatia maoni ya Wananchi.
5.USHIRIKIANO,-Kufanya kazi kwa pamoja katika maswala ya msingi kwa maslah ya Nchi.
6.MUUNGANO,-Kuulinda muungano bila kuwa na migongano ya maslahi kama ilivyo sasa.
7.UZALENDO,-Kuhimiza
na kusimamia ushirikiano wa pamoja baina yao na makundi mbalimbali bila
kuweka mbele maslah yoyote ya vikundi na kuhakikisha Wananchi wanapata
Tanzania mpya.
No comments:
Post a Comment