Meneja masoko wa Tusker Lager Anitha Msangi akiongea na wasambazaji wa biaza SBL kwenye uzinduzi wa kampeni ya Tusker Fanya Kweli mjini Moshi.
Meneja biashara ukanda wa ziwa Avinash akiongea na wasambazaji wa bia za SBL katika uzinduzi wa kampeni ya Tusker Fanya kweli mjini Mwanza.
Meneja wa bia ya Tusker Lager Sialouise N Shayo na wasmabazaji wa bia za SBL pichani wakionyesha muonekano mpy wa bia ya Tusker Lager katika uzinduzi wa kampeni ya Tusker Fanya kweli mjini Mwanza.
Meneja usalama na Afya Emmanuel Ntoma akiongea na wasambazaji wa bia za SBL mjini Moshi katika uzinduzi wa kampeni ya Tusker Fanya Kweli Mjini humo.
Meneja masoko Orest Mbaga akiongea na wasambazaji wa bia za SBL katika uzinduzi wa kampeni ya Tusker Fanya kweli mjini Moshi.
Meneja masoko Orest Mbaga na wasamabzaji wa bia za SBL katika uzinduzi wa kampeni ya Tusker Fanya kweli mjini Moshi.
Baada
ya kuzindua kwa mafanikio kampeni ya Tusker “Fanya Kweli” jijini Dar es Salaam hivi karibu, kampuni ya bia ya
Serengeti imezindua tena kampeni hiyo katika mikoa ya Mwanza na Kilimanjaro.
Fanya Kweli ni kampeni itakayoendeshwa na
kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake cha Tusker Lager na
itaendeshwa nchi nzima. Lengo la kampeni hii ni kubadilisha fikra za watanzania
ili wawe na shauku ya kujituma katika kujitafutia maendeleo yao ili nao waishi maisha
bora.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo jijini Mwanza, Meneja Chapa wa Tusker,
Sialouise Shayo alisema, “Kampeni hii ya fanya Kweli imelenga kuwawezesha
watanzania kupata fikra mpya za kimaendeleo ili kufikia malengo waliyojiwekea,”
shayo aliwaambia wakazi wa Mwanza kwamba Fanya Kweli ipo ili kuwawezesha
kufikia malengo yao.
Katika
hali tofauti kampeni ya Fanya Kweli pia imezinduliwa Moshi ambapo kampuni ya
bia ya Serengeti kupitia chapa yake ya Tusker imezindua kampeni kama hiyo kwa
wakazi wa Moshi.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo mjini Moshi Meneja Masoko wa kampuni ya bia ya
Serengeti, Anitha Msangi alisema “kampeni ya Fanya Kweli ina maana kuamsha
mwamko mpya na kubadili fikra za watanzania na leo tunawaambia wakazi wa Moshi
kuwa ndoto yoyote uliyonayo itafanikishwa”.
Katika kuhakikisha watanzania wanailewa vizuri
kampeni hiyo, Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti, Ephraim
Mafuru alisema “Tunatarajia kuwa na programu katika redio zitakazoendeshwa kwa
wiki ambapo watu waliofanya kweli katika sekta mbalimbali wataongelea
matatizo,vikwazo walivyokumbana navyo katika safari yao ya kufanya kweli, jinsi
gani waliweza kuyatatua na ni wadau gani waliwasaidia kuweza kuvishinda vikwazo
hivyo. Pamoja na kampeni hiyo, wanywaji wa bia ya Tusker watapata nafasi ya
kushuhudia Fanya Kweli katika promosheni zitakazofanyika kwenye baa mbalimbali,
vyombo vya habari na “application” itakayowawezesha wanywaji wa Tusker
kujumuika kwa pamoja.
No comments:
Post a Comment