Na
Felix Mwagara, Nachingwea
WAZIRI wa Mambo ya
Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe
ametangaza rasmi kuwa atagombea tena katika nafasi ya ubunge kupitia CCM katika
uchaguzi Mkuu ujao na kulitetea jimbo lake. Alisema hayo juzi alipokuwa
akizungumza na wananchi pamoja na viongozi wa CCM wa Wilaya na Kata ya Mtua,
wilayani Nachingwea katika sherehe ya kuwapokea viongozi na wanachama wapya wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliojiunga na CCM wilayani humo.
Waziri Chikawe alisema
wananchi wake bado wanamuhitaji kwa hiyo hawezi kuacha kugombea nafasi hiyo
kwani wazee na wananchi mbalimbali katika Kata zote alizokuwa akipita kufanya
mazungumzo nao wanamuomba agombee tena nafasi hiyo.
“Wakati nikiingia ubunge
mwaka 2005 katika jimbo hili kulikuwa hakuna lami na barabara nyingi za kwenda
vijijini zilikuwa hazipitiki na pia maji yalikuwa shida lakini sasa barabara za
lami mjini Nachingwea zimejengwa, maji yanapatikana tena yasio na chumvi,
barabara vijijini zinapitika kwa kuwa zimechongwa vizuri kwa kuwawezesha
wakulima kupitisha mazao yao,” alisema Chikawe huku akishangiliwa na mamia ya
wananchi waliofurika katika sherehe hiyo.
Picha/Story
na Felix Mwagara.
No comments:
Post a Comment