Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday, 4 October 2014

WANAJESHI 9 WA UMOJA WA MATAIFA WAUAWA


Mwanajeshi wa Umoja wa Mataifa
Ujumbe wa Umoja wa mataifa nchini Mali unasema kuwa watu waliokuwa na silaha ambao walikuwa wakitumia pikipiki wamewaua walinda amani tisa wa Umoja wa Mataifa kaskazini mashariki mwa taifa hilo.
Uvamizi huo ndio mbaya zaidi kuwai kuwakumba wanajeshi hao wa Umoja wa Mataifa.

Wanajeshi hao kutoka nchini Niger walikuwa wakisafiri kati ya miji ya Menaka na Ansongo wakati walipovamiwa.
Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa amesikitishwa na kile alichokitaja kuwa vitendo vya kigaidi.
Mwandishi wa BB nchini Mali amesema kuwa kikosi hicho cha umoja wa mataifa kimelalamika kuhusu vifaa duni inavyomiliki.
Walindamani hao walitumwa miaka miwili iliyopita baada ya makundi ya wanamgambo wa kiislamu kuchukua udhibiti wa maeneo ya kaskazini mwa Mali.
CREDIT: BBC/SWAHILI

No comments:

Post a Comment